NI mwenye kujiamini, maadili mema. Rais mpya wa Botswana, Duma Boko, ndivyo anavyotafsiriwa hivyo nchini mwake.
Amepata ushindi kwa kuking’oa chama kilichokuwa mamlakani. Boko mwenye umri wa miaka 54, amebobea kwenye haki za binadamu na ni wakili.
Elimu yake ya uanasheria ilianzia nchini mwake, hatimaye kwenda Shule Kuu ya Sheria Harvard, huko Marekani.
Huyo ni Boko, mbali na unyenyekevu wake baada ya ushindi, ameushangaza umma wa dunia, kutokana na kuvunja dhana kwa wapinzani kwamba haiwezekani.
Kwa miaka 50 upinzani wa kisiasa nchini humo, wamekuwa wakiota ndoto, kukivua madaraka chama kikuu cha Botswana Democratic Party, lakini ni Boko pekee ndiye aliyefanikisha hilo.
Mbinu ya ushindi wa chama chake cha Umbrella for Democratic Change (UDC) ilishangaza. Yeye mwenyewe Boko, amekiri kushtushwa na idadi hiyo ya kura za ushindi.
Akiwa amevalia suti rangi ya bluu iliyokolea, hakuonesha kufurahi au kusherehekea kwa nguvu kwa maoni yake ya kwanza kwa vyombo vya habari siku ya Ijumaa, licha ya wakati ukubwa wa ushindi alioupta na wake kudhihirika rasmi.
“Ninaweza tu kuahidi (kwa watu) nitafanya kila niwezalo. Nitakaposhindwa, nitawatazama wao, waniongoze.”
Boko amebainisha wazi nchi inakopita ikiwamo changamoto za kiuchumi kwa ahadi ya kuleta mabadiliko katika ajira na mishahara serikalini.
Mbinu zake kwenye kampeni zilimbeba. “Watu walimpenda na haya ndiyo matokeo yake,” mwanahabari Innocent Selatlhwa aliiambia podcast ya BBC Focus on Africa.
Katika muda wote wa kampeni yake, mikutano ya hadhara, Boko alikuwa akiwaomba wafuasi wake kuja karibu na kuwasikiliza malalamishi yao, ni njia ambayo ilimfanya kuwavutia vijana.
Alionekana ni mzito, lakini Boko alikuwa akivutia kila wakati na mwenye urafiki.
Pia alikataa kugombea kama mbunge na kuweka juhudi zake zote kuwa rais kwa ujasiri.
Alizaliwa mwaka 1969, katika Wilaya ya Kati nchini humo, katika mji mdogo wa Mahalapye. Boko daima alikuwa na hisia ya heshima, kulingana na marafiki.
"Alivutiwa sana na kufanya jambo sahihi. Hisia zake za haki zilienea sana,” shangazi yake aliliambia gazeti la mtaani.
Wakati wa shule, alichaguliwa kuwa rais wa baraza la wanafunzi. Katika taaluma yake ya sheria, aliibuka kuwa mmoja wa wanasheria wakuu nchini, kulingana na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Lesole Machacha.
“Anamaanisha na yuko makini kuweka vizuri nchi,” aliongeza.
Alikua kiongozi wa Chama cha Kitaifa cha Botswana (BNF) mwaka 2010, ambacho kilikuwa na "itikadi za kikomunisti" zaidi, alisema Bw Machaha, lakini chama hicho tangu wakati huo kimeelekea kwenye kituo hicho.
Kutokana na vyama vya upinzani kushindwa kwa miongo mitano, Boko aliunda muungano wa vyama vinavyopinga serikali na UDC ikazaliwa.
Alikashifiwa zaidi ya muongo mmoja uliopita alipowaelezea wafanyakazi wa kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Botswana kama "wasiofaa", licha ya kuwa alikuwa mhadhiri hapo awali zamani.
Watu wengi walichukulia hili kama kuuchimba mfumo wa elimu nchini humo. Alipoulizwa kuhusu hilo na mwandishi wa habari katika kituo cha habari cha Afrika Kusini eNCA alijibu: "Ukweli unauma."
Mapema mwezi huu, mkewe, Kaone Boko, aliliambia gazeti liitwalo told the Mmegi kwamba mumewe huwa harudi nyuma kwenye jambo lake analolisimamia.
“Huwa harudi nyuma, anapigana, bila kujali afui yake ni mkubwa kiasi gani.”
Chama chake ni miongoni kati ya vilivyofanikiwa barani Afrika.
Chama tawala cha Botswana BDP cha Rais Mokgweetsi Masisi kimeshindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 30, mwaka huu.
Ushindi huo unahitimisha miaka 58 ya utawala wa chama hicho madarakani.
Tayari Rais Mokgweetsi Masisi amekiri kushindwa kwenye kinyang'anyiro hicho, baada ya matokeo kuonesha kuwa chama chake kimepoteza wingi wa viti bungeni.
Masisi amesema ameshazungumza na kiongozi wa chama cha upinzani cha mrengo wa kushoto cha UDC cha mgombea, Duma Boko, ili kupanga namna ya kukabidhi madaraka.
Ushindi wa upinzani nchini humo ambao haukutarajiwa ni pigo kubwa chama tawala na Masisi aliyeingia madarakani mwaka 2018. Chama chake kimekuwa madarakani tangu Botswana ilipopata uhuru kutoka kwa Uingereza, mnamo mwaka 1966.
Zaidi ya watu milioni moja walijiandikisha kupiga kura katika uchaguzi huo kati ya raia milioni 2.6 wa taifa hilo.
Chama kilichoshinda cha UDC kilianzishwa na Boko mnamo mwaka 2012, kwa nia ya kuunganisha makundi ya upinzani dhidi ya chama tawala.
Hii ni mara ya tatu kwa Boko ambaye pia ni mwanasheria kuwania Urais. Aidha baada ya matokeo ya awali kupitia ukurasa wake wa Facebook kiongozi huyo wa upinzani aliandika "mabadiliko yamewadia".
Kando ya kupata wingi wa viti bungeni chama cha Boko kimepata pia ushindi mkubwa katika uchaguzi tofauti wa serikali za mitaa.
Wingi wa viti vya bunge umeupa ushindi upinzani Kulingana na televisheni ya taifa, chama cha UDC kimeshinda viti 26 kati ya 61 vinavyowaniwa wakati chama tawala cha BDP kikiwa na viti viwili pekee.
CHANZO: DW/BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED