BENKI ya Stanbic Tanzania imezindua kampeni ya “Tap Kibingwa” ili kuhamasisha malipo ya kidigitali kupitia Kadi za Visa Debit.
Kampeni hiyo itawafanya wateja kupata nafasi ya kushinda zawadi za kuvutia, ikiwa ni pamoja na zawadi za fedha za TZS 300,000 na 500,000 kila mwezi, na zawadi kuu ya gari jipya aina ya Suzuki Fronx na mapumziko ya kifahari ya siku tatu Zanzibar.
Alisema kampeni hiyo, inalenga kukuza matumizi ya malipo kupitia mashine za POS na eCommerce kwa ajili ya uzoefu wa usalama, urahisi, na manufaa.
Kampeni hii itakayoendeshwa kuanzia Januari 10 hadi Machi 31, 2025, inawahamasisha wateja kutumia Kadi zao za Visa Debit kwa miamala ya POS na eCommerce ili kushinda zawadi za kuvutia.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Omari Mtiga, Mkurugenzi wa Wateja na Huduma Binafsi wa Benki ya Stanbic, alisema
“Katika Stanbic, tumejidhatiti kukuza mtindo wa maisha wenye usalama, urahisi, na zawadi kwa wateja wetu. Kampeni ya ‘Tap Kibingwa’ inaakisi dhamira hii, kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kupitia miamala rahisi ya kidigitali huku tukiwapa zawadi za kuvutia. Tunakaribisha kila mtu kushiriki nasi katika safari hii ya uwezeshaji wa kifedha.”
Alisema wateja watakaofanya miamala angalau 50 yenye thamani ya Sh 30,000,000 au zaidi ndani ya kipindi cha kampeni watahitimu kushiriki droo kuu kushinda gari jipya aina ya Suzuki Fronx na mapumziko ya kifahari ya siku tatu Zanzibar kwa wawili.
Irene Mutahibirwa, Meneja wa Kitengo cha Kutoa Kadi wa Benki ya Stanbic, alisisitiza kuhusu zawadi:
“Kampeni hii haihusu tu miamala. Ni kuhusu kuwathamini wateja wetu na kuwapa nafasi ya kushinda zawadi za kuvutia. Kuanzia zawadi za fedha hadi zawadi kuu ya gari jipya aina ya Suzuki Fronx na mapumziko Zanzibar, tunafurahia kusherehekea wale wanaokubali malipo ya kidigitali pamoja nasi.”
Ili kuongeza msisimko wakati wa uzinduzi, dereva maarufu wa mashindano ya magari, Dharam Pandya, alitoa maoni yake kuhusu gari la Suzuki Fronx:
“Suzuki Fronx si gari tu; ni ishara ya ubora na ujasiri. Ni zawadi kamili kwa mtu yeyote anayekubali urahisi wa miamala ya kidigitali. Nimefurahi kuwa sehemu ya kampeni hii na kushuhudia jinsi Stanbic inavyounda mustakabali wa malipo nchini Tanzania.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED