WAZIRI wa Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema serikali imepanga kuimarisha Mawasiliano kwa kuunganishwa mtandao wa mkongo wa Taifa kutokea nchi jirani ya Kenya.
Waziri Silaa ameyasema hayo leo katika eneo la mpaka wa Horohoro alipokagua mradi wa ufikishaji wa mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kutokea Mombasa, nchini Kenya.
Amesema kwa sasa mkongo umeweza kuunganishwa na nchi nyingine jirani za Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na Kenya, huku jitihada kubwa inafanyika kufikisha huduma hiyo katika nchi za Congo na Msumbiji.
"Kuimarika kwa mawasiliano ya kimtandao kutawezesha nchi yetu kuweza kukuwa kiuchumi lakini na wananchi watu wataweza kufikia huduma za kimataifa ikiwemo masoko kwa uharaka na uhakika" amesema Waziri Silaa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED