WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Dk. Ashatu Kijaji, ameagiza kufungwa kwa viwanda na maduka yote yanayojihusisha na nyavu zisizofaa kwenye shughuli za uvuvi ikiwa ni hatua ya kukomesha uvuvi haramu nchini.
Akizungumza jana (Disemba 19, 2024) wakati wa ziara yake mkoani Mara baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Uvuvi mkoani humo iliyobainisha kwa kiasi kikubwa changamoto ya Uvuvi haramu.
Alisema kuwa moja ya jukumu lake kubwa wakati wote atakaohudumu kwa nafasi yake ni kuhakikisha anarejesha hali ya upatikanaji wa samaki nchini kama ilivyokuwa awali ili kuokoa viwanda vya kuchakata samaki vilivyopo nchini .
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ametangaza awamu nyingine ya kupambana na uvuvi haramu mkoani humo itakayoanza mwezi Januari mwakani ambapo amewataka wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja huku akiwatahadharisha kutomlaumu pindi atakapoanza kutekeleza operesheni hiyo.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED