Kocha Mkuu wa timu ya MC Alger, Khaled Benyahya muda huu akizungumza na vyombo vya habari kuelekea mchezo wao wa kesho Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi dhidi ya Yanga mchezo ambao utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Akizungumzia mchezo huo amesema mchezo huo utakuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa.
"Mechi itakuwa na ushindani lakini tumejipanga vema kuhakikisha tunapata pointi tatu licha ya Dar kuwa na joto kali, amesema Ben Yahya.
Kwa upande wake Zakaria Draoui ambaye amezungumza kwa niaba ya wachezaji amesema amejipanga vizuri kupata ushindi licha ya kuwepo na upinzani.
"Kwa upande wetu Tunafahamu ni mchezo ambao utakuwa na upinzani hivyo lazima tuingie kwa tahadhari, amesema Draoui
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED