KOCHA Mkuu wa Klabu ya Yanga Saed Ramovic akizungumzia maandalizi kuelekea Mchezo wao wa kesho dhidi ya MC Alger (Algeria) utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Amesema amejipanga vizuri kuhakikisha anapata pointi tatu ili aweze kuingia hatua ya robo fainali.
"Mchezo utakuwa mgumu kesho tunapaswa kupambana tuweze kufunga kwani tukipoteza safari yetu itakuwa imeishia hapo, amesema Ramovic
Amesema morali ya kila mchezaji ipo vizuri jambo ambalo linampa matumaini makubwa na kuwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuwasapoti wachezaji wao.
Kwa upande wake Dickson Job ambaye amezungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema wapo tayari kupata matokeo katika mchezo huo.
"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo tukiwa kwenye uwanja wetu wa nyumbani tunaomba mashabiki waje kutushangilia bila wao hatuwezi kufanya lolote, amesema Job.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED