ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiaskofu la Anglikana Duniani (ACC) nchini Tanzania, Elibariki Kutta ameahidi kujenga uwanja mkubwa wa kisasa wa mpira kwa miguu katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ikiwa ni jitihada za kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya michezo.
Askofu Kutta ametoa ahadi hiyo jana, alipokuwa mgeni rasmi katika mchezo wa soko uliowahusisha vijana wa eneo la Mlali wilayani Kongwa, ambapo katika hotuba yake ameahidi kuboresha sekta ya michezo kwa kujenga uwanja wa kisasa ili kusaidia vipaji vya vijana viendelezwe.
Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na vipaji vya vijana wengi kucheza soka lakini vikwazo ni mazingira kutowasaidia kutimiza ndoto zao, ameongeza uwepo wa kiwanja hicho kwa vijana wa Kongwa utawasaidia kuibua na kuviendeleza vipaji vyao.
“Mbali na kujikita kuisaidia serikali kuboresha sekta ya Elimu, Maji, Afya lakini pia tutasaidia masuala ya michezo, tumeamua kufanya hivyo kwa sababu napenda kushirikiana na serikali kuwaletea maendeleo wananchi,” amesema Askofu Kutta.
Askofu Kutta, septemba 15 mwaka huu mkoani Dodoma, anatarajiwa kukabidhiwa rasmi majukumu ya kuongoza kanisa hilo nchini Tanzania, viongozi mbalimbali wa kanisa hilo duniani akiwamo Askofu Mkuu duniani, Mark Haverland.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED