Vikwazo vinavyonyonya juhudi za wanawake kuwania nafasi za uongozi

By Neema Emmanuel , Nipashe
Published at 03:42 PM Aug 13 2024
Vikwazo vinavyonyonya juhudi za wanawake kuwania nafasi za uongozi.
Picha: Neema Emmanuel
Vikwazo vinavyonyonya juhudi za wanawake kuwania nafasi za uongozi.

UONGOZI ni ushawisishi,dhana na taaluma inayompa mtu madaraka ya kuunganisha nguvu na anaowaongoza ili kuleta maendeleo na kuifikia malengo yao walioyatarajia.

Hivi ndivyo juhudi za wanawake kuwania nafasi kwa changuzi katika ngazi mbalimbali unavyopigwa marufuku kwa nguvu ndani ya jamii hofu ya ushiriki ubaguzi ,rushwa, upendeleo wa kijinsia,mila na desturi kandamizi ni moja ya vikwazo vinavyochochea Wanawake kuwa nyuma na kutokuwania nafasi mbalimbali za uongozi huku takwimu za Uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa kwa ngazi ya mtaa vijiji na vitongoji kote nchini wanawake hawakuzidi hata asilimia 28  ya wanaume.

Hiyo inaweza kuletana athari kubwa kwa vizazi vijavyo na kwa wale wanaojitahidi kushiriki katika chaguzi inaweza kusababisha kupinga juhudi za wanawake kwa sababu ya kutokuelewa faida zinazoweza kupatikana huku wengine wakikata tamaa ya kushiriki wakihofia kushindwa ama kutokupewa ushirikiano.

Sundi Charles ni mkazi wa Kijiji cha Ihayabuyaga wilayani Magu akizungumza na Nipashe Digital anaeleza kuwa yeye ni mama wa  nyumbani hana elimu yoyote ya uongozi hivyo amejikita katika kilimo, ufugaji na kulea watoto .
" Napenda kuwa kiongozi sina elimu hiyo ata nikisema nikagombee kwenye uchaguzi unaokuja wa serikali za mitaa najua siwezi kupata sina hela ata mme wangu awezi kunikubalia " anaeleza.

Aidha Semeni Kasori mjasiliamali kutoka Kijiji cha Matela anaeleza kuwa tatizo ni jamii hasa wanaume kutokuwa na imani na Wanawake kuwa wanao uwezo wa kuongoza  hiyo inachangia kuwa na idadi ndogo ya wagombea wa njinsia ya kike.

" Japo kuwa Rais katufungulia njia kwa upande wangu naupenda uongozi lakini naogopa lawama za watu huku kwetu kuna wakati  wanamlalamikia  mwenyekiti amekula fedha za miradi ukweli mimi naogopa sipendi kukosana na watu au kutuhumiwa vitu visivyo na ukweli " anaeleza Kasori .

Naye Mariam Iddi mkazi wa Isangijo kisesa anaeleza kuwa Wanawake wenye ulemavu ukiwemo wa ngozi wanachukiliwa kama watu dhaifu ambao hawawezi uongozi labda wapewe nafasi za upendeleo ,alitoa wito kwa jamii kuacha ubaguzi na kuwa na haki sawa ili kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali.

1

Anaeleza ili kuwa kiongozi lazima kujitoa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi japokuwa kufikia nafasi yoyote inahitaji moyo na uvumilivu mkubwa kwa sababu majaribu ni mengi na wakati mwingine ukatisha ndoto ama dhamira ya wanawake kujitoa katika kugombea nafasi mbalimbali.

Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea haki za wasichana na Wanawake (KIVULINI) Yassin Ally anaeleza kuwa Tanzanian ni moja ya nchi iliyopiga hatua sana katika kuleta usawa wa kijinsia na wanawake kushiriki uongozi ambapo imefanikiwa sana ngazi za juu ikiwemo wabunge,mawaziri , Rais,Spika na wakuu wa Wilaya na wanafanya vizuri  hiyo inatosha kudhiilisha wanawake wanaweza .

Anaeleza kuwa tatizo lipo kwenye kugombea nafasi ngazi ya mtaa, vijiji na vitongoji wanawake wapo nyuma kujitokeza tofauti na wanaume hivyo ni wakati wao kujitokeza kwa wingi kwa sababu eneo ilo la serikali za mitaa  lipo karibu sana na wananchi ndilo kimbilio la kwanza la ulinzi na  usalama kwa watu pia ni kiungo kikubwa cha ustawi wa  maendeleo hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kufikia malengo.

"Kwanini kwenye uongozi wa ngazi za juu tunafanya vizuri na huku chini kuwa ni changamoto? Shida iliyopo ni mfumo wa chaguzi wa ndani ya vyama vya siasa ambapo wagombea lazima wapitishwe na vyama vyao hilo ni tatizo hasa kwenye kura za maoni.

Naviomba vyama vya siasa nchini vyenye dhamira ya kuleta mapinduzi viweke mkakati mahususi wa kuhakikisha wagombea wanawake wa ngazi za vitongoji, vijiji na mitaa wenye sifa na vigezo wanajitokeza na waweze kushindanishwa kihalali" anaeleza
2

Anaongeza kuwa tatizo lingine ni matumizi ya fedha katika chaguzi ambapo amesema kwa sababu uchaguzi unahitaji pesa na siyo lazima kwa ajili ya kuhonga wajumbe bali ata mtu akienda kufanya mkutano wa adhara ataitaji spika kwa ajili ya sauti na vitu vingine.

Kasema kuwa changamoto ni katika ngazi ya kaya ambapo wanawake wanachangia kikamilifu katika uzalishaji kipato na uchumi ngazi ya kaya tatizo anaye amuavipi pesa hiyo itumike ni baba, mama hana haki ya kutumia pasipo ruhusa.

" Nawaomba wanaume na wanawake watambue nafasi za kuchaguliwa kisiasa kwanza zinaimalisha uchumi wa kaya na uchumi wa nchi hivyo ni vyema familia zikatoa ushirikiano kwa watoto,wake wenye uwezo wa kuongoza ipasavyo wakashiriki kugombea nafasi mbalimbali,” aliongeza ndugu Ally.

Anasema kuwa mabadiliko ya kisheria wakati huu yamekuwa na wigo mpana ambapo wadau wa haki za wanawake wanahakikisha masuala ya ukatili wa kijinsia hasa wa kingono uliokuwa ni tatizo kubwa wakati wa uchaguzi yamezingatiwa hivyo anawaomba vijana ,wanawake ni hatimu yao ya kushika uongozi kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa .

Vyama vyote vya siasa wakati wamefanya mabadiliko ya kanuni,sheria na taratibu za uchaguzi walihakikisha zinatoa fursa kwa mwanamke na pia ni vyema kanuni ndani ya vyama zihakikishe zinakuza ushiriki na fursa pana za wanawake wenye sifa na vigezo kuweza kushika nafasi hizo kwa sababu serikali za mitaa ndilo kimbilio la kwanza la wanawake na watoto hususani wanaotendewa ukatili uwe wa kiuchumi ama vipigo ni vyema kuwe na uwiano mzuri wa wanawake katika ngazi hizo.
3

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Sauti ya Wanawake Ukerewe, Sophia Donald, ameeleza kuwa kupitia majukwaa yao watahamasisha wanawake wajitokeze kushiriki katika kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuelekea kwenye uchaguzi waweze kupiga kura na kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali.

Akizungumza Jijini Mwanza katika ufunguzi wa mkutano wa Tume na wadau wa Uchaguzi Mwenyekiti wa INEC Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele  anaeleza kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) mkoani Mwanza inatarajia kuandikisha wapigakura wapya 190,131 ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.3 ya wapiga kura zaidi ya milioni 1.8(1,845,816),waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na matarajio yake baada ya zoezi hilo Mkoa huo utakuwa na wapiga kura milioni 2,035,947.

Alisema Tume imepewa jukumu la kutoa elimu ya mpiga kura nchini hivyo watu wenye ulemavu,wajawazito na akinamama wajitokeze kwa wingi kujiandikisha pia wamejipanga kuhakikisha kuwa wananchi wanapata uelewa wa kutosha na wajitokeze kwa wingi kushiriki zoezi hilo.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ( INEC) Ramadhani Kailima, ameeleza kuwa idadi ya vituo vya kuandikisha wapiga kura kwa mwaka 2024 nchini vitatumika 40,126 kati ya hivyo 39,709 vipo Tanzania Bara na 417 vipo Zanzibar ni ongezeko la vituo 2,312 ikilinganishwa na vituo 37,814 vilivyotumika 2019/2020.

“Kwa Mkoa wa Mwanza vitatumika 2,251 kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 73 katika 2,178 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/2020,” alisema.

Aidha Mjumbe wa Kamati ya Siasa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wazazi mkoani humo Mohammed Lukonge anaeleza kuwa elimu inatolewa ya kuwahamasisha Wanawake kujutokeza kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuanzisha kampeni ya "Tukutane kwa Balozi" wapo mtaani kutoa hamasa hiyo kwa akinamama wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.
4

Akizungumza suala zima la utolewaji wa rushwa hasa ya ngono katika vipindi vya uchaguzi anaeleza kuwa jambo hilo halipo hivyo wanawake wajitokeze kwa wingi kuomba nafasi mbalimbali kwani CCM inatoa kimaumbile na kuhakikisha wanawake wanashiriki katika kutoa mchango wao wa kiuongozi katika nyanja zote kuanzia shina mpaka ngazi za kitaifa.

Anaeleza kuwa dhana ya jamii kuwapa vipaumbele wanaume katika uongozi awali mfumo dume ulikuwepo na ndio utamaduni waliokuwa wanaimani nao mfumo huo uliwanyima fursa wanawake lakini kwa sasa haupo.

"Kiongozi siyo lazima awe mwanaume lakini toka chama kilivyo mpendekeza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa makamo wa Hayati John Magufuli hapo ndipo tulipoanza kufuta ile dhana ya kwamba mwanamke hawezi kuongoza lakini sasa mmeweza kuona namna Rais wa Tanzania mwanamke  anavyoongoza zaidi ya watu million 60 na anafanya vizuri katika uongozi hivyo wanawake wasiowe na hofu wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali zinapojitokeza" anaeleza Lukonge.
5