WAZIRI wa Mipango na Uwekezaji,Prof.Kitila Mkumbo,amesema serikali ya Tanzania haitakuwa kikwazo kwa Asasi za kiraia nchini, bali watatoa ushirikiano ili kuhakikisha wanapeleka maendeleo kwa wananchi.
Pia amezitaka asasi za kiraia kutafuta na kutumia fursa ya rasilimali zilizoko nchini kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.
Waziri Prof.Kitila,alisema hayo jana jijini Arusha,wakati wa akifungua wiki ya Azaki kwa mwaka 2024, inayofanyika kwa siku tano na washiriki wako zaidi ya 600.
Alisema kuna umuhimu kwa mashirika hayo yasiyokuwa ya kiserikali kushirikiana na serikali ikiwamo kutoa maoni na kukaa meza moja kutaua matatizo yanayowakibili wananchi kwa kuwa itasaidia kukuza uchumi wa nchi na kuwakwamua kiuchumi.
Hata hivyo,alisema serikali itahakikisha ustawi wa mwananchi mmoja mmoja unakuwa na ili kufika lengo hilo,kila mtu anapaswa kutoa maoni chanya katika uandaaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.
Alisema endeapo Azaki kwa kushirikia na wananchi watatoa maoni italeta tija hasa katika suala la uwekezaji katika sekta za elimu,afya,maji,umeme,barabara,utalii,madini,ufugaji na kilimo.
“Hadi sasa asilimia 81 ya vijana kati ya miaka 15 mpaka 35 wameshatoa maoni mbalimbali kuhusiana Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,hivyo tunatambua kwamba kuna changamoto kwenye suala la uchumi,lakini mnapaswa kufanya tathimini wapi nchi ilipotoka na tuendako,”alisema Prof.Kitila.
Aidha alitaka mashirika hayo,kuisema jami kutokana na changamoto zinazowakabili ili kutafutwa kwa njia mbadala za utatuzi badala ya kuilalamikia serikali kwamba haifanyi kazi.
Naye Rais wa Foundation For Civil Society (FCS), Dk. Stigmata Tenga,alisema ili kutokea kwa mabadiliko YA kiuchumi kwa Watanzania ni lazima yatokane na uwepo wa Azaki ambazo zina jukumu na kuwasemea wananchi wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali.
Mkurugenzi wa TradeMark Africa,Elibariki Shammy,alisema mpango mkakati uliowekwa na serikali ni kuhakikisja biashara za kidigitali zinakua zaidi kwa kushirikisha vijana.
Alisema wanashiri kwa kasi kubwa katika biashara kwa kuweka mazingira wezeshi yatakayowasaidia wananchi wakiwamo vijana kujikaua kiuchumi kutokana na fursa zilizoko nchini.
Awali Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya(EU),Isabelle Mignucci, alishukuru ushikiano uliopo kati serikali ya Tanzania na mashirika mbalimbali ya kiraia.
Alisema ushirikiano huo,unaleta tija katika mpango wa maendeleo kwa kuwa utasaidia sauti za vijana zinasikika ikiwemo kutafuta fursa za maendeleo kupitia teknolojia na ubunifu kwa ukuaji wa uchumi kupitia shughuli wanazofanya vijana hasa kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHEMA).
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED