Uturuki kushambulia penye ukame Syria, milioni moja walia na maji

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:05 AM Nov 20 2024
Hali halisi ya shida ya maji maeneo ya ukame, Syria.
PICHA: MTANDAO.
Hali halisi ya shida ya maji maeneo ya ukame, Syria.

INAELEZWA kuwapo mashambulizi ya anga kutoka Uturuki katika eneo lililokumbwa na ukame Kaskazini- Mashariki mwa Syria, yamesababisha uhaba wa upatikanaji wa umeme na maji kwa zaidi ya watu milioni moja.

Sasa wataalamu wanasema, huenda kuwapo ukiukaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na washamhuliaji hao, tangu Oktoba mwaka 2019 hado kufika Januari mwaka huu. 

Ni ushambulizi unaotekelezwa katika maeneo yenye mafuta, mitambo ya gesi na vituo vya umeme yanayoshikiliwa na jamii za Wakurdi huko Kaskazini na Mashariki mwa Syria.

Pia, mashambulizi hayo yanatajwa kuongeza hali mbaya ya kibinadamu katika eneo linalokumbwa na vita vya wenyewe vilivyodumu kwa miaka mingi, pia ukame mkubwa kwa miaka minne unaochangiwa na mabadiliko ya tabianchi.

Maji yantajwa yalikuwa kidogo, mashambulizi dhidi ya miundombinu ya umeme mwezi Oktoba mwaka jana yalikatisha umeme na kukatisha maji katika kituo kikuu cha maji cha eneo hilo, huko Alouk na hakifanyi kazi tangu wakati huo.

Serikali ya Uturuki inatajwa ililenga vyanzo vya mapato vya vikundi vya Wakurdi vinavyotaka kujitenga ambavyo vinahesabiwa kuwa ni vikundi vya kigaidi.

In ataja mahali hapo panajulkana kuna ukame na kuongeza kuwa usimamizi mbovu wa maji na miundombinu umesababisha hali kuwa mbaya zaidi.

Zaidi ya watu milioni moja katika mkoa wa Hassakeh ambao hapo awali walipata maji kutoka eneo la Alouk, sasa wanategemea maji yanayosukumwa kutoka umbali wa maili 12, sana na kilomita 20.

JANGA LA MATETEMEKO

Mapema mwaka huu, Umoja wa Mataifa kupitia vyombo vyake ikaripotiwa kuwa mwaka mmoja baada ya matetemeko makubwa ya ardhi yaliyokumba Uturuki na Syria, Umoja wa Mataifa ukatamka mamilioni ya manusura waliokumbwa na matetemeko hayo pamoja na wenyeji waliowapatia hifadhi inazidi kudorora.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwamo la kuhudumia wakimbizi – UNHCR na lile la afya, WHO ikatoa tathmini hiyo kupitia wasemaji wake jijini Geneva, Uswisi.

Shabia Mantoo, Msemaji wa UNHCR anafafanua: “Uturuki ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa kuhifadhi wakimbizi, ilhali Syria nayo ambako mamilioni ya watu wamefurushwa makwao kutokana na janga la miaka 13 sasa hata kabla ya tetemeko, inakumbwa na janga kubwa la kiuchumi.”

Akaongeza: “Nchini Syria takribani asilimia 90 ya watu ni mahohehahe, milioni 12.9 hawana uhakika wa kupata chakula ilihali milioni 7.2 ni wakimbizi wa ndani."

Matetemeko hayo ya ardhi yanatajwa yaliikumba eneo la mpakani mwa nchi mbili hizo, Februari mwaka 2023 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 50,000 nchini Uturuki na zaidi ya 5,000 Kaskazini-Magharibi mwa Syria na maelfu wengine walijeruhiwa.

Uharibifu huo unatajwa ulikuwa mkubwa, kwa maelfu ya majengo, yakiwamo ya miundombinu muhimu kama shule na hospitali yaliporomoka kutokana na ukubwa wa tetemeko.

“Uturuki inahifadhi wakimbizi milioni 3.4, na tetemeko la ardhi limeathiri eneo ambalo ni makazi ya wakimbizi milioni 1.75,” akasema, Msemaji anawajibika na wakimbizi.

Ofisa huyo wa UNHCR, akataja kuwapo madhara ya matetemeko yako dhahiri kwa wakimbizi na wenyeji wao.

Anaongeza kuwa, kutokana na ongezeko la mahitaji, wakimbizi wengi wakaamua kutumia mbinu mbadala za kuishi, ikiwemo kupunguza mlo na kukopa fedha zaidi.

“Janga hili tayari limekuwa na madhara kwenye afya ya akili na ustawi wa jamii husika. Watu wengi wamepoteza familia na marafiki,” anasema  Mantoo.

Kwa upande wa WHO, inaelezwa kuwa madhara ya tetemeko hilo yatadumu kwa miaka kadhaa ijayo ambapo watu wengi wataendelea kuishi kwenye makazi ya muda.

“Nchini Uturuki, tetemeko limesababisha uwepo wa mahitaji mapya na ya dharura ya kiafya kwenye jamii zilizoathiriwa, ikiwamo kwa wakimbizi na wenyeji,” anasema Tarik Jasarevic, Msemaji wa WHO.

Anaongeza kuwa janga hilo lilivuruga namna ya kufikia huduma za afya kwa wahitaji kama vile wajawazito na watoto wachanga, pia huduma za chanjo, usimamizi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, afya ya akili, na huduma kwa watu wenye ulemavu.

Kwa zaidi ya muongo mzima, Syria imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo mzozo uliodumu muda mrefu, ukosefu wa utulivu kiuchumi, janga la afya kama vile Covid -19, kipindupindu na sasa tetemeko la mwaka jana la ardhi.

Kutoka ofisi ya Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, OSE, Jenifer Fenton, anatamka: “Baada ya matetemeko ya ardhi tumeshuhudia kiwango cha chini kabisa cha uhasama na mwelekeo mpya wa kidiplomasia katika janga la Syria. 

“Hata hivyo, haikuleta maendeleo halisi. Kwa kusikitisha, mwaka 2023 umeshuhudia kuibuka upya na kwa kiasi kikubwa kwa mapigano, na hivyo kufanya hali ya kibinadamu kuwa mbaya zaidi na ukosefu wa mchakato wa maana wa kisiasa.”

·      Kwa mujibu vyanzo tofauti