INAPOTANGAZWA dhana inayohusiana na huduma ya dharura hospitalini, hapo inagusa sura kuu kadhaa, kuwahisha kunusuru hai wa mgonjwa aliye taabani.
Hiyo yaweza kuanzia anavyofikishwa kwa matibabu, anahudumiwa na safu ya wataalamu na watumishi tib ana nyenzo zinazotumika. Ni mara zote sura ya tiba kwa mgonjwa hunaziona anapoingia mikononi mwa matabibu.
Iwe ni kwa ajali au sababu nyinginezo kama ujauzito, mgonjwa huanza kuona sura ya ahueni safari yake kwenda kituo tiba inaanza, anapofikishwa katika mlango qwa kituo tiba, mikononi mwa wataalamu wanatumia aina nyenzo, iwe miundombinu kama vitanda na vile vya maabara.
Katika hilo, ndio Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameamua kulishikia kibwebwe kama sehemu ya mipango yake kuimarisha huduma ya afya kitaifa.
Zamani, msamiati “majengo ya kutoa huduma za dharura’ au (EMD) kuwapo sana, sasa ni sehemu ya hospitali nchini, Wizara ya Afya ikiwa na ufafanuzi katika taarifa yake kipindi kama hiko mwaka jana kwamba:
“Miaka mitatu ya Rais Samia imewezesha kuanzishwa kwa majengo mahususi ya huduma za dharura na ajali (EMDs) 105 kutoka EMD saba zilizokuwapo mwaka 2020.’
Ufafanuzi wa Wizara ya Afya, unagusa maeneo ya hospitali maalum kama ya (Jakaya Kikwete – JKCI, Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili – MOI za Dar es Salaam; pia Benjamin Mkapa, Dodoma), za kanda kama Mbeya na mikoa kama vile; Kigoma na Lindi, pia wilaya kama Handeni.
“Kukamilika kwa ujenzi wa EMD kutapunguza vifo na kuokoa maisha kwa wagonjwa wa dharura na wa ajali kwa asilimia kati ya 40-50 kwa mujibu wa tafiti za kitaalam.” Inafafanua Wizara ya Afya.
MAGARI WAGONJWA
Ni hatua inayoendana na kipindi hicho nchini kuingiza magari ya wagonjwa 727 mwaka mmoja uliopita, ikilenga kurahisisha utoaji wa huduma za matibabu ya dharura kwa wagonjwa wahitaji katika hali mbaya.
“Yamepelekwa na kusambazwa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini...” anatamka taarifa hiyo yenye ufafanuzi:
“Zinakwenda kusaidia kusafirisha wagonjwa, wakiwamo kinamama wenye changamoto za uzazi kwa haraka na kuwafikisha katika huduma za rufani, hivyo kupunguza adha kwa wananchi na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika.”
RASILIMALIWATU TATIZO
Katika mtazamo huo wa huduma dharura -EMD, mafanikio yake hukamilishwa na jitihada za wataalamu wanaowajibika mahali hapo pa afya.
Hapo ikumbukwe kuwa katika tafsiri ya utendaji tiba duniani, inaegemea kinachoitwa ‘Labour Oriented Capital’, nguvukazi inataegemewa zaidi, kuliko mitambo, tofuti na ‘Capital Oriented’; kunakotegemewa zaidi mitambo, kuliko rasilimaliwatu.
Hivyo, kuwapo safu inayotosha kwa idadi na stadi za kiutendaji, ina maana kubwa kwa ufanisi wa tiba ya mgonjwa na mahsusi huduma hiyo ya dharura.
Mgonjwa wa dharura anayochukuliwa na gari, huanza kupata huduma tiba pindi angiapo katika gari husika, ambako kunakuwapo wataalamu na huduma za dharura kumhudumia, akiwa safarini kwenda hospitalini.
Hilo ni eneo moja linalomsukuma Rais Dk. Samia katika zama za uongozi wake, kuajiri wataalamu kusaidia dharua na huduma nyingine, kupitia kauli za Wizara ya Afya mwaka jana:
“Jumla ya wataalamu 35,450 wa kada mbalimbali wameajiriwa na kusambazwa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2023. Aidha, jumla ya ajira za mikataba kwa watumishi wa Afya 2,836 kupitia miradi mbalimbali ya serikali zilitolewa...’
Wizara ya Afya inafafanua kutumia shilingi bilioni 22 hadi mwanzoni mwa mwaka jana, zikiwa ni jitihada za kusaidia kupata wataalamu mabingwa wa afya kwa fani tofauti, watakaotumika kujenga uwezo wa wataalamu wengine nchini katika vyuo vya mafunzo ya afya.
“Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuimarisha upatikanaji wa wataalamu wabobezi kwa ajili ya utoaji wa huduma za Kibingwa na Ubingwa Bobezi, kwa kuanzisha Dk. Samia ‘Super Specilized Scholarships’.
“Hadi sasa jumla ya wataalam 1,211 wamepata mafunzo mbalimbali ya kibingwa na bobezi...jitihada hizo zitaimarisha upatikanaji wa huduma hizo za kibingwa bobezi ambazo zitawezesha nchi kunufaika na tiba utalii,” inaelekezwa katika ripoti hiyo.
Zinatajwa nchi za kigeni wanufaika wa tiba utalii ni Comoro, Burundi, Malawi, Kenya, Congo DRC, Uganda na Zambia.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, safu ya wataalamu wanufaika mafunzo kati ya mwaka 2021 an 2024, wameongezeka kutoka 535 wa mwaka 2021 wakati Dk.Samia anaingia madarakani, hadi wataalamu 1,211 kwa mwaka wa sasa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED