MWANZO wa msimu wa kusuasua kwa Real Madrid umechangiwa na jeraha baya alilopata beki wa kati, Eder Militao.
Miezi ya mwanzo ya kampeni imetawaliwa na mwanzo mgumu wa maisha ya Bernabeu kwa usajili wa majira ya kiangazi wa Kylian Mbappe na kutoswa kwa Vinicius Junior katika tuzo za Ballon d'Or, lakini kazi ya 'Los Blancos' ya kurudisha ubora wao wa kutetea mataji ya LaLiga na Ligi ya Mabingwa Ulaya imefanywa kuwa ngumu zaidi, kwa pigo aliloacha Mbrazil huyo.
Hatacheza tena msimu huu, na kumwacha Kocha Carlo Ancelotti akikosa chaguo huku David Alaba akiendelea kupata nafuu kutokana na tatizo lake la misuli.
Baada ya kumkosa Leny Yoro aliyekwenda Manchester United na kuachana na mpango wa kumsajili nahodha wa zamani Sergio Ramos, Madrid inaweza kulazimika kuingia kwenye soko la usajili Januari ili kurekebisha safu yao ya ulinzi.
Hawa hapa ni baadhi ya mabeki ambao wanaweza kuwalenga kwenye dirisha la majira ya baridi ili kukabiliana na kukosekana kwa Militao...
#6. Jarrad Branthwaite
Jarrad Branthwaite amelazimika kushughulika na matatizo yake ya majeraha hadi sasa msimu huu, akianza mechi mbili tu za Ligi Kuu kutokana na tatizo la paja.
Ana mambo mengi ya kufanya ikiwa anataka kuibuka kama chaguo la kweli kwa 'Los Blancos', bila shaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ni kipaji ambaye angeendana na mkakati wa Madrid wa kusajili wachezaji wachanga na wazuri.
Inaweza kuwa hatari kwa sasa ukizingatia rekodi yake ya utimamu wa mwili na akiwa bado hajaonesha kiwango cha juu, lakini bado anastahili kuzingatiwa.
#5. Cristian Romero
Unapojaribu kubaini safu dhabiti za ulinzi, pengine si wazo kuu kuwaangalia Tottenham Hotspur.
Hata hivyo, Spurs ina beki wa kati aliyeshinda Kombe la Dunia, Cristian Romero, ambaye inasemekana ana mashabiki wake huko Madrid.
Litakuwa jambo la kufurahisha sana kwa mchezaji huyo wa Kimataifa wa Argentina kushirikiana na Antonio Rudiger, lakini huenda ikatakiwa kutolewa ofa kubwa zaidi Januari ili kumnasa kutoka Kaskazini mwa London.
#4. Castello Lukeba
Beki wa RB Leipzig, Castello Lukeba amekuwa mmoja wa majina ya kwanza yaliyopendekezwa na vyombo vya habari vya Hispania kupunguza jeraha la Militao.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ufaransa mara moja amejijengea sifa ya kuwa mlinzi mgumu wa upande wa kushoto, aliwasili Saxony mwaka jana akitokea Lyon baada ya Josko Gvardiol kwenda Manchester City.
Bahati mbaya kwa Madrid, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, amesaini mkataba mpya wa kuongezwa na Leipzig, ambao umeongeza kifungu chake cha kuruhusiwa kuondoka hadi kufikia euro milioni 90.
Miamba hao wa Bundesliga hakika hawatataka kumuuza Lukeba kwa punguzo la fedha hiyo, na kuwaacha mabingwa hao wa Hispania katika hali ngumu ya mazungumzo.
#3. Jonathan Tah
Ingawa Lukeba angekuwa usajili wa gharama kutoka Ujerumani, Jonathan Tah anaweza kupatikana kwa bei nafuu zaidi.
Mkataba wa sasa wa beki huyo unamalizika mwishoni mwa msimu huu, akihusishwa na kuhamia Ligi Kuu England, huku pia akiwaniwa na Barcelona.
Bayern Munich pia wametajwa kama mahali panapotarajiwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, lakini Madrid wanaweza kuharakisha mbinu ya kumnunua mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ujerumani.
#2. Vitor Reis
Kwa kuzingatia mafanikio ya Real Madrid katika kunyakua vijana wenye vipaji kutoka Brazil, haishangazi kwamba nyota wa Palmeiras, Vitor Reis ameibuka kama chaguo linalowezekana Januari.
Kinda huyo aliwaniwa sana na Madrid wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi na anaonekana atajiunga na magwiji hao wa Ulaya siku za usoni, baada ya kuguswa na uchezaji katika safu ya ulinzi.
Mchezaji ambaye anafananishwa na nyota wa Paris Saint-Germain, Marquinhos, Reis ni kipaji kingine cha kutumaini ambacho kinaweza kutumika kwa Ancelotti wakati wa uhitaji wake.
#1. Laporte Aymeric
Ramos hatarejea Bernabeu, lakini Aymeric Laporte anafikiriwa kuwa mmoja wa walengwa wakuu wa Madrid Januari.
Beki huyo wa zamani wa Manchester City hajaonesha dalili za kuruhusu viwango vyake kushuka licha ya kutimkia Saudi Arabia, akiwa na mchango mkubwa Hispania iliposhinda Euro 2024 majira ya joto.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED