FRELIMO yaibuka kidedea RENAMO, wapinzani wenza watupwa mbali

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 09:58 AM Oct 16 2024
Mshindi wa urais Msumbiji Daniel Chappo wa FRELIMO  na mgombea huru asiyefungamana na chama chochote kwenye urais huo, Venancio Mondlane.
PICHA ZOTE: MTANDAO
Mshindi wa urais Msumbiji Daniel Chappo wa FRELIMO na mgombea huru asiyefungamana na chama chochote kwenye urais huo, Venancio Mondlane.

MGOMBEA Daniel Chapo, wa chama kikongwe cha siasa Msumbiji cha FRELIMO, ameshinda kiti cha urais katika majimbo mengi makubwa ya nchi hiyo pamoja na mji mkuu Maputo.

Baada ya kutawala Msumbiji tangu uhuru mwaka 1975, kimetawala miaka 50, kilielezwa kuzoa  asilimia 53.68 ya kura zilizopigwa Maputo. Mwingine ni Venâncio Mondlane mtoto wa mpigania uhuru Edward  Monndlane, akipata asilimia 33.84, akifuatiwa na Ossufo Momade wa RENAMO, aliyepata takriban asilimia tisa wakati Lutero Simango wa chama cha MDM akiwa na asilimia tatu.

Itakumbukwa kuwa Eduardo  Mondlane alikuwa mwanamapinduzi  na mwanaharakati wa ukombozi wa Msumbiji, ambaye ni mwanzilishi wa Chama cha Ukombozi cha Msumbiji FRELIMO. Alikuwa kiongozi wa kwanza wa FRELIMO hadi alipouawa mwaka 1969 nchini Tanzania na wapinga ukombozi wa Afrika.

 FRELIMO ni miongoni mwa vyama vikongwe barani Afrika na kimedumu mamlakani kwa takribani nusu karne.

Upinzani umepinga matokeo hayo katika maeneo yalikotangazwa hasa majimbo makubwa baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita Oktoba 9.

Nickson Katembo, mchambuzi wa kisiasa akiwa nchini humo anasema wananchi walio wengi hawakutarajia matokeo hayo.  Chapo kupitia FRELIMO katika uchaguzi huu, amegombea akimrithi Rais anayemaliza muda wake, Filipe Nyusi.

Mpinzani wake mkuu ni Ossuo Momade, kutoka RENAMO, wengine walikuwa ni Lutero Simango wa MDC na mgombea binafsi Venâncio Mondlane.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (CNE), zaidi ya watu milioni 17 walijiandikisha kupiga kura, wakiwamo 333,839 wanaoishi nje ya nchi.

FRELIMO, ilishinda kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka 2019 baada ya kupata asilimia 73 ya kura zilizopigwa, japo  RENAMO, ilitupilia mbali ushindi huo kwa madai ya kukosa imani na mchakato wote.

Kwa mujibu wa Radio DW, bado hakuna matokeo rasmi, lakini inadhihirika wazi kuwa FRELIMO, chama kilichokuwa madarakani tangu uhuru mgombea wake, Chapo, atashinda.

Katika kinyang'anyiro cha urais, Mondlane, mmoja wa wagombea watatu wa upinzani aliondoka RENAMO na kuwania kama mgombea binafsi, dhidi ya mwenyekiti wa RENAMO, Ossufo Momade.

Mondlane anadai ni mwathirika wa udanganyifu mkubwa katika uchaguzi: "Tunachokiona hapa ni wizi wa hali ya juu kabisa wa uchaguzi," anaiambia DW na kuongeza: "Hili si jambo jipya, tumeona hili chaguzi zilizopita."

Katika eneo lenye utulivu la kaskazini mashariki la Cabo Delgado, ambalo limevumilia vita vya umwagaji damu vya wanajihadi tangu 2017, Chapo pia alishinda rasmi, kwa takriban asilimia 66 ya kura, akifuatiwa na Mondlane asilimia 22.64.

Momade alishika nafasi ya tatu kwa asilimia 7.56 na Lutero Simango alimalizia mwisho, kwa chini ya asilimia nne.

"PODEMO, chama ambacho bado hakijawakilishwa bungeni ambacho kilimuunga mkono Mondlane kuwania urais, kitachukua nafasi ya RENAMO," mchambuzi wa Msumbiji Jaime Guiliche aliiambia DW.

"Nadhani tutaona hali ambayo Renamo si tena nguvu ya pili kwa ukubwa wa kisiasa na itaanguka hadi nafasi ya tatu. Hiyo ingekuwa mabadiliko makubwa katika mazingira ya kisiasa ya nchi yetu," Guiliche anasema.

Uchaguzi mkuu wa Jumatano ulijumuisha uchaguzi wa saba wa kiti cha urais kwa nchi hiyo, Rais Filipe Nyusi, amefikia kikomo cha kikatiba cha mihula miwili, hajashiriki.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, matokeo ya majimbo yanapaswa kuhesabiwa hadi mwisho wa leo, huku hesabu katika wilaya zote 154 za nchi ikiwa imekamilika mwishoni mwa wiki.

Kwa matokeo hayo ambako tayari yametangzwa, hakuna duru ya pili, huchukua hadi siku 15 (kuhesabiwa tangu kufungwa kwa kura), kabla ya kupitishwa kuthibitishwa na Baraza la Katiba, ambalo hakuna tarehe ya mwisho ya kutangaza matokeo rasmi baada ya kuchanganua rufani zinazowezekana.

Kura hiyo ilijumuisha uchaguzi wa wabunge wa bunge la kitaifa (manaibu 250) na wa mabunge ya majimbo na magavana wao husika na viti 794 vitagawanywa.