Wananchi Igonia wapata zahanati,Waziri Silaa awapa kongole DED,DC kwa usimamizi

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 01:03 PM Oct 25 2024
Wananchi Igonia wapata zahanati,Waziri Silaa awapa kongole DED,DC kwa usimamizi
Picha: Mpigapicha Wetu
Wananchi Igonia wapata zahanati,Waziri Silaa awapa kongole DED,DC kwa usimamizi

WANANCHI zaidi ya 1,400 wa vijiji vya Igonia, Ikungu na Mtamba wilayani Mkalama mkoani Singida wataondokana na adha ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 10 hadi kijiji cha Mkalama kufuata huduma za matibabu kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati ya Igonia ambayo imegharimu Sh. milioni 87.4.

Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, ambaye alizundua zahanati hiyo jana, alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama,Asia Messos na Mkuu wa Wilaya hiyo, Moses Machali kwa kusimamia vizuri ujenzi wa zahanati hiyo ambayo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kabla ya serikali kuongeza nguvu.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, aliwataka wananchi kudumisha upendo na ushirikiano kwa watumishi ili waweze kuwa na ari na moyo wa kufanya kazi. Miradi mingine aliyotembelea waziri ni mradi wa maji katika kijiji cha Nkalakala uliogharimu Sh.milioni 348.9.

3