TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, imefanikiwa kuokoa Sh. milioni 66 za makusanyo ya POS mashine, zilizokuwa hazijapelekwa benki katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Victor Swella, amesema hayo leo, Januari 29, 2025 jijini hapa na wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya taasisi hiyo, kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba, mwaka jana, mbele ya waandishi wa habari.
Swella amesema katika kuhakikisha inasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato katika halmashauri za mkoa wa Dodoma, imekuja na utaratibu wa kupata taarifa za makusanyo ya POS, kwa kila halmashauri kwa siku ya Jumatatu.
Amefafanua kuwa lengo la kufanya hivyo ni pamoja na kubaini kama kuna makusanyo ambayo hayajapelekwa benki kama utaratibu unavyotaka, ili kuchukua hatua mapema ya kudhibiti hali hiyo kabla ya ubadhirifu mkubwa kufanyika.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED