Waziri Lukuvi atoa mitungi ya gesi kwa vijana

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:59 AM Sep 30 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) William Lukuvi
Picha:Mpigapicha Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) William Lukuvi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) William Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Isimani ameendelea kuunga mkono kampeni ya kutumia nishati safi ya kupikia kwa kutoa majiko ya gesi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi ya kata ya mpira wa miguu katika jimbo la Isimani.

Waziri ametoa majiko hayo kwa washindi wa nafasi ya kwanza, nafasi ya pili na nafasi ya tatu wakati alipotembelea kata Mlenge Mkoani Iringa jana katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo katika vijiji vya Magombwe, Isele, Kinyika na Kisanga vilivyopo katika kata ya Mlenge .

“Majiko 1200 yanatarajiwa kutolewa kwa washindi wa mpira wa miguu kwa kata zote za jimbo la Isimani ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Mhe, Rais Dk, Samia Suluhu Hassani katika kutumia nishati safi ya kupikia,” alisema Waziri Lukuvi.

Katika hatua Nyingine Waziri Lukuvi, ameomba wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuendelea kuunga mkono serikali utekelezaji na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa.

Ameongeza kusema utakapofika muda wa uandikishaji kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani, naomba vijana wenye umri wa miaka 18 na kuendelea mjitokeze kujiandikisha  uchaguzi wa Mwakani muweze kupiga kura.