Watafiti waumiza kichwa kumwangamiza mbu aenezaye chikungunya

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 03:47 PM Aug 29 2024
mbu aina Aedes.
Picha: Mtandao
mbu aina Aedes.

WATAALAM na watafiti masuala ya afya kutoka nchi mbalimbali duniani wamekutana nchini kujadili namna ya kuja na njia ya pamoja ya kupambana na magonjwa yanayoenezwa na mbu aina Aedes.

Mbu hao wanaeneza magonjwa aina ya dengi, chikungunya na manjano.

Hayo yalisemwa Jana jijin Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti  Wadudu Wanaoeneza Magonjwa kutoka  Wizara ya Afya, Charles Mwalimu   katika mkutano huo.

Alisema utafiti ambao tayari umefanyika umebaini  mabadiliko ya hali ya hewa ndio sababu ya kuzaliana kwa mbu hao kwa wingi.

Alisema dalili zake hazina tofauti na zile za malaria akisisitiza walioko katika hatari ya kupata maambukizi ni wale wanaoacha sehemu kubwa za miili yao wazi.

Alizitaja njia za kujikinga na magonjwa hayo kuwa zinajumuisha kujisitiri, kupaka mafuta yenye dawa ya kuzuia mbu kung'ata, kufanya usafi wa mazingira na kuangamiza mazalia yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Afya Ifakara,(IHi) Honorati Masanja alisema mbu hao wanapatikana zaidi mijini.

"Hawa mbu hata ukiangalia kwenye mpango wa kitaifa wa malaria utaona dalili zake zinaingiliana na zile za malaria" alisema Masanja