Wananchi waaswa kuiunga mkono serikali matumizi Nishati safi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:04 PM Oct 10 2024
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Advera Mwijage.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Advera Mwijage.

Wananchi wametakiwa kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kuhakikisha wanahama kutoka kwenye matumizi ya nishati chafu ya kupikia, inayosababisha madhara ya kiafya,kimazingira na kiuchumi na kuanza kutumia nishati safi ili lengo kuu la kutumia nishati safi kwa asilimia 80 ifikapo 2034 liweze kufikiwa.

Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Advera Mwijage ameyasema hayo wakati wa Semina maalum ya nishati safi ya kupikia iliyotolewa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa wananchi wa ya Bukombe.

Mwijage amesema katika kuhakikisha wananchi wanaondoka kwenye nishati chafu ya kupikia Serikali imetoa ruzuku kwenye mitungi ya gesi ili kila mwananchi aweze kumudu bei na kuingia kwenye  nishati safi ya kupikia.

Alisema hadi sasa mitungi 85,000 tayari imesambazwa sehemu mbalimbali nchini,na kwa awamu ya pili wamelenga kusambaza mitungi 452,445 kwa mikoa yote nchini huku kila Wilaya ikipata mitungi 3500.

Wilaya ya Bukombe ni mopa ya Wilaya iliyoanza kunufaika na ruzuku hiyo ambapo katika semina hiyo mitungi zaiid ya 1600 ilitolewa kwa bei ya ruzuku ya Sh17,500.

 Akizungumza kwenye semina hiyo iliyolenga kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, Mratibu wa Nishati Safi ya kupikia kutoka Wizara ya Nishati  Ngereja Mgejwa alisema lengo la Serikali ni kuona matumizi ya nishati safi ya kupikia inapanda kutoka asilimia 10 zilizopo sasa hadi kufikiaasilimia 80 ifikapo 2034.

1

Mgejwa alisema zipo imani potofu kuwa kupika kwa kutumia gesi husababisha chakula kisiwe kitamu na vingine kutoiva vizuri na kuwataka waachane na imani hizo potofu. 

Alisema matumizi ya nishati chafu ya kupikia husababisha madhara ya kiafya,kimazingira na hata kiuchumi huku akisema takwimu zinaonyesha watu 33,000 hupoteza maisha kutokana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia. 

“Kutokana na changamoto hizo Serikali imeamua kuingia kwenye nishati safi ya kupikia kwa kuanzisha mkakati wa miaka kumi wa kuhakikisha asilimia 80 ya watanznaia wanatumia nishati safi ya kupikia”amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Paskasi Muragili  amesema upatikanaji wa mitungi ya gesi inayotolewa kwa ruzuku ni mabadiliko chanya kwa nishati ya kupikia kwa wananchi. 

Baadhi ya wananchi waliopatiwa majiko ya nishati safi ya kupikia Ester James amesema matumizi ya kuni mbali na kusababisha madhara kiafya lakini huwafanya kina mama kutumia muda mwingi kupika tofauti na matumizi ya gesi.

2