MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umewatunuku Wafanyakazi wake Bora kwa mwaka 2023/24 katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Mfuko huo jijini Dodoma.
3
Aliyeongoza shughuli ya utoaji tuzo ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Abdul-Razaq Badru.
Waliotunukiwa ni pamoja na Mfanyakazi Bora wa Kwanza, Yasinta Christopher , Mfanyakazi Bora wa Pili ni Fatma Elhady na mfanyakazi aliyeshika namba tatu ni Gideon Mswashihongo.
Aidha Badru pia alimpa tuzo Mfanyakazi wa PSSF ambaye amefikia muda wa kustaafu John Shayo.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED