Ulega ataka kasi ya kijeshi miradi ya dharura

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:36 PM Dec 19 2024
Ulega ataka kasi ya kijeshi miradi ya dharura.

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka mameneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuogeza spidi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara. Ulega amewaambia mameneja hao kuwa wanatakiwa waende kwa spidi inayofanana na viwango vya kasi vinavyoonekana wakati Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapopewa majukumu ya utekelezaji na serikali kwa sababu kuna mvua zinakuja na zinaweza kufanya maeneo yaliyoharibika kuharibika zaidi.