DC Apson : Wananchi msiwe na hofu Daraja la Nkuhi halijakatika

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 06:04 PM Dec 19 2024
MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Thomas Apson.

MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Thomas Apson, ametoa ufafanuzi kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa daraja lililopo kijiji cha Nkuhi wilayani humo limekatika na kusababisha kuwepo kwa foleni ya magari yaliyokuwa yakisafiri kutoka Dodoma kwenda Singida na Mwanza.