Tundu Lissu: Uongozi wangu utajikita kwenye haki

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 01:03 PM Jan 29 2025
Tundu Lissu: Uongozi wangu utajikita kwenye haki.
Picha:Halfani Chusi
Tundu Lissu: Uongozi wangu utajikita kwenye haki.

Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kuwa uongozi wake utajikita zaidi katika kuhakikisha haki inatendeka ndani ya chama na kwa wananchi kwa ujumla.

Lissu ametoa kauli hiyo leo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na kuanza majukumu yake kama mwenyekiti wa chama.

"Hatutamuonea mtu yeyote. Tutahakikisha tunafanya kazi kwa pamoja na kwa haki," amesema Lissu.

Aidha, amewahimiza wale wanaotaka kujiunga na CHADEMA wasisite kufanya hivyo, akisisitiza kuwa chama kinahitaji nguvu kubwa zaidi ili kufanikisha malengo yake.

"Tunahitaji jeshi kubwa mara mbili ya lililopo sasa. Tunahitaji kila mtu alete karama zake na baraka alizopewa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kazi hii," amesema.

Pia, Lissu amewataka wanachama na wafuasi wa chama hicho kushiriki kwa hali na mali katika kuimarisha chama, akisema kuwa mchango wa kila mmoja unahitajika.

"Ninawakaribisha wote wanaotaka kutusaidia, iwe kwa mafuta ya gari, pesa au rasilimali nyingine. Kazi hii inahitaji ushirikiano wa kila mmoja wetu," amesisitiza Lissu.