TALIRI kutafiti mbegu tano za malisho ya mifugo

By Grace Mwakalinga , Nipashe
Published at 05:39 PM Jul 08 2024
Mwakilishi wa Kampuni ya Afrint Bio Solution Limited   nchi za Afrika,  Emmanuel Paluku akitoa elimu kwa wananchi  juu ya virutubisho  ya wanyama wafugwao wanavyovizalisha bila kutumia kemikali,waliotembelea banda la Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania
Picha: Mpigapicha Wetu

TAASISI ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), inaendelea na utafiti utakaosaidia urasimishaji wa aina tano za mbegu bora za malisho ambazo zitatumiwa na wafugaji kwa ajili kuzalisha chakula cha mifugo na hivyo kuongeza tija ya uzalishaji.

Hatua hiyo ni miongoni mwa jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, wanyama wafugwao wakiwa ni miongoni mwa wanaozalisha hewa ya ukaa kwa sababu ya chakula kisicho bora  wanachokula ambacho mmeng'enyo wake husababisha wanyama kutoa kinyesi kinacholeta hewa ya ukaa ukilinganisha na malisho yaliyonoreshwa ambayo yanarahishisha mmeng'enyo

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania TALIRI, Prof. Erick Komba ametoa  kauli hiyo wakati wa maonesho  ya sabasaba alipozungumza na Nipashe Digitali kuhusu hatua mbalimbali walizozichukua katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya  tabianchi.

Prof. Komba amesema  kuwa miongoni mwa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni  taasisi hiyo kubuni mbegu za malisho bora ambazo zitakazo sambazwa kwenye maduka yote ya pembejeo za mifugo ili zitumike na wafugaji kwa kuanzisha Mashamba ya malisho kwa ajili ya mifugo yao.

“Tuna kwenda kuhamasisha wafugaji wetu kutenga maeneo ya mashamba ya kuzalisha malisho bora kwa ajili ya mifugo yao, ukipiga hesabu ekari 2.5 ya shamba la malisho bora inahudumia ng'ombe mmoja kwa mwaka na akastawi vizuri kabisa ukilinganisha na akitumia malisho ya asili, tunahimiza watumie malisho yaliyoboresha ambayo yamefanyiwa utafiti na Taliri, amesema  Prof. Komba.

Ameongeza  kuwa malisho hayo yaliyoboreshwa yatakuwa mwarobaini wa kukabiliana na migogoro ya wakulima na wafugaji kwani wafugaji watakuwa na malisho ya kutosha.

Kwa upande wake , Mtafiti Mwandamizi wa mifugo kutoka TALIRI,  Gilbert Msuta amesema  wameendelea kufanya utafiti  wa malisho kwa ajili ya wanyama kwa kushirikiana na wadau wa mifugo ndani na nje ya nchi.

Amesema  miongoni mwa wadau wanaoshirikiana na TALIRI ni Shirika la Afrint Bio Solution Limited ambao wanazalisha virutubisho vya asili vya mimea, mifugo na samaki kutoka nchini Indonesia.

Ameongeza  kuwa wamefanya utafiti kwenye bidhaa hizo na kuangalia uhalisia kabla ya kwenda kwenye mifugo na kudai kwamba matokeo ya awali yanaonesha virutubisho hivyo vinasaidia  kwenye ukuaji wa mifugo kama vile ng'ombe kuku na nguruwe.

“Matokeo ya virutubisho vya mdau wetu kutoka Indonesia vimeonyesha kuwa havina madhara wala kemikali badala yake inasababisha mnyama kukua haraka na kuwa na uzito mkubwa kwa vile vinasaidia mmeng'enyo wa chakula. Tunahamaisha na wadau wengine wa sekta ya mifugo kuleta bidhaa ambazo zitasaidia kwenye utafiti na ustawi wa mifugo yetu,” amesema  Msuta.

Naye mwakilishi wa Kampuni ya Afrint Bio Solution Limited   nchi za Afrika,  Emmanuel Paluku amesema kuwa ilianza kuingiza bidhaa zake nchini mwaka  2018 na kwamba hadi sasa zaidi wa wafugaji milioni moja wametumia bidhaa za kampuni hiyo.

Amesema  lengo la kuanzisha bidhaa hizo ni kupunguza matumizi ya kemikali vinavyopatikana kwenye viuadudu na viuatilifu vinavyotumika kwa wanyama na mimea ambavyo vimetajwa kusababisha madhara kwa watumiaji kama vile kansa.

Ameongeza   kuwa bidhaa wanazozalisha zimekidhi viwango vya kimataifa vya uzalishaji wa virutubisho visivyo na kemikali na  kusaidia ukuaji haraka wa wanyama.

“Bidhaa zetu za asili ambazo zinazalishwa kwa kutumia teknolojia ya Nano ambayo haiathiriki na inamudu vipindi vyovyote iwe, mvua, au jua na virutubisho hivyo huuzwa kwa gharama nafuu na matokeo yake ni ya muda mfupi, mfugaji atanufaika kwa kuuza mifugo kwa bei nzuri,” amesema  Paluku .

Aidha kupitia maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya saba saba yanayofanyika jijini Dar es Salaam, wameandaa bidhaa zenye virutubisho mbalimbali kwa ajili ya kusaidia mifugo  na mimea.