JULAI mwaka huu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imesherehelea maadhimisho ya miaka 22 tangu ilipoanzishwa Julai, 2002.
Hata hivyo, bado wachambuzi wa masuala ya siasa na kimataifa wanahoji namna malengo ya mahakama hiyo, huku wakijiuliza maswali kuhusu upendeleo unaonekana dhidi ya mataifa ya Afrika, athari zake kwa uhuru wa kitaifa, na madai ya maelekezo ya kisiasa.
Waangalizi wa kimataifa nao mashaka kama nchi za Afrika na zile za Kusini mwa Dunia kweli zinafaidika na taasisi hii ambayo msingi wake unaonekana kufanya haki kwa kuchagua, kuzitolea macho nchi za Afrika, na kuacha mataifa yenye nguvu kukwepa uwajibikaji.
Zaidi ya miongo miwili iliyopita wakati ilipoanzishwa jijini Roma, ICC ilileta matumaini kwa ajili ya siku zijazo za sheria za kimataifa kwani wengi walidhani ingekuwa kiongozi wa kesi za uhalifu wa kivita.
Nchi zote za Amerika Kusini na idadi kubwa ya nchi za Afrika zilisaini mkataba wa Roma unaoanzisha ICC, wakiwa na imani na malengo ya kimsingi kwamba ICC itawafikisha wahalifu wa ukatili wa kivita, mauaji ya kimbari, na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Haki za Kimataifa (GJC), Elise Keppler, anasema ndoto kuu ilikuwa kwamba ICC itatoa haki kwa wahasiriwa.
Anasema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilianzisha mahakama mbili zenye lengo la kuhukumu uhalifu uliofanyika Rwanda na Yugoslavia ya zamani.
Viongozi 120 waliokutana Roma, Italia walikubali kuanzishwa kwa ICC ili kuichukua mahakama hizi za muda.
Wakati wa maadhimisho ya ICC, Julai, 17 mwaka hii Rais wa ICC, Jaji Tomoko Akane aliliambia jopo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) New York kwamba. “Mwongozo wetu pekee ni sheria inayohusika, ambayo kwanza na muhimu ni mkataba wa Roma, uliotungwa kulinda ubinadamu. Kila mtu ni sawa mbele ya sheria na hakuna mtu aliye juu ya sheria."
Mshauri wa kisheria kuhusu haki za kibinadamu na sheria za kimataifa kutoka Shirika la Amnesty International, Melissa Hendrickse, anasema rasimu za kuzuia na kutoa hukumu dhidi ya uhalifu wa binadamu ziliandaliwa na Tume ya Sheria za Kimataifa (ILC) kati ya mwaka 2013 na 2019.
Anasema baadaye zilipelekwa katika Kamati ya Sita ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jukwaa kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuzingatia masuala ya kisheria.
Elise anabainisha kwamba hitaji la uelewa mkubwa kuhusu makala za rasimu ni kubwa hususani Afrika.
Anasema Afrika ina idadi kubwa ya nchi ambazo bado hazijaeleza wazi kama makala za rasimu zinapaswa kuendelea hadi majadiliano.
Anasema nchi pekee zilizoonyesha nia katika hati hiyo ni Sierra Leone, Afrika Kusini, na Gambia.
Anasema nchi ya Ghana, Angola, Mozambique, Guinea-Bissau, São Tomé na Príncipe, Guinea ya Ikweta, Cabo Verde, Senegal, na Tunisia zimeonyesha tu kuunga mkono. Akisema hii inamaanisha hazijawasilisha maoni yao kwa maandiko.
Anasema nchi kama Zambia, Malawi, Lesotho, Namibia, Botswana, Benin, Liberia, Ivory Coast, na Uganda, hazijachukua msimamo rasmi kuhusu suala hili.
Elise anasema “Mkataba wa uhalifu dhidi ya ubinadamu utakuwa tofauti na Mkataba wa Roma wa ICC. Utashughulikia uwajibikaji wa mataifa kuzuia na kuadhibu uhalifu tofauti na ICC inayoshughulikia uwajibikaji wa kibinafsi.”
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED