Aweso aelekeza kasi utekelezaji miradi ya maji miji 28

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:18 PM Aug 13 2024
Aweso aelekeza kasi utekelezaji miradi ya maji miji 28.
Picha: Mpigapicha Wetu
Aweso aelekeza kasi utekelezaji miradi ya maji miji 28.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Mhandisi Arnab Saha Menaja Mkazi wa Kampuni ya WAPCOS LTD akiwa ni Mkandarasi Mshauri na Msimamizi wa Miradi ya Maji ya Kimkakati ya Miji 28 Ofisi za Wizara ya Maji Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.

1Lengo na dhumuni la kikao hicho ni Mhandisi Arnab kujitambilisha baada ya Meneja mkazi wa awali wa Kampuni hiyo kumaliza muda wake na pili kutoa taarifa fupi ya maendeleo ya miradi inayotekelezwa maeneo mbalimbali nchini.

Pia Aweso amemjulisha Mhandisi mshauri kwamba amepanga ziara ya kupita nchi nzima kuikagua na kuifiatilia miradi hiyo na itaanza hivi karibuni.

Aidha, Waziri Aweso ametumia fursa ya kikao hicho kutoa pongezi kwa kazi kubwa na nzuri inayoendelea na zaidi kutoa maelekezo mahususi na kuagiza kuongezwa kwa kasi ya utekelezaji wa Miradi ya Miji 28 kwasababu wananchi katika maeneo hayo wamekua na changamoto ya Maji kwa muda mrefu sana na ni wakati sahihi wa kupata huduma hii kwa haraka na kueleza zaidi kwamba fedha za miradi hii zipo hivyo ni lazima wakandarasi kupambane usiku na mchana, kuongeza kasi kukamilisha kazi na akisisitiza kwamba hayo ndio maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.

Katika hatua nyingine Mhandisi Arnab amemhakikishia Aweso kwamba atafanyia kazi maelekezo haya namiradi katika miji mbalimbalj kazi itakamilika mapema kama yalivyo matarajio na maelekezo ya Waziri kila anapopita kukagua miradi hiyo katika ziara zake wilaya mbalimbali nchini.