Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imeziandikia barua nchi zote 16 wanachama kuomba uungwaji mkono kwa mgombea wa Madagascar katika kinyang’anyiro cha kumrithi Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) Moussa Faki.
Kinyang’anyiro hicho kina wagombea watatu: Raila Odinga wa Kenya, Richard Randriamandrato wa Madagascar na Mahamoud Ali Youssouf wa Djibouti.
Jamhuri ya Madagascar imeibuka kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya SADC kuwania nafasi hiyo baada ya Mauritius kujiondoa katika ugombea wake.
Hilo ni pigo kwa juhudi za viongozi wa ukanda wa Afrika Mashariki kumpigia kampeni mwanasiasa huyo mkongwe na waziri mkuu wa zamani wa Kenya kurithi mikoba ya Moissa Faki.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED