WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Dk. Ashatu Kijaji ameiagiza Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kuongeza wigo wa uzalishaji wa mbegu bora za mifugo na malisho ili kuongeza upatikanaji wa nyama nchini na kukuza uchumi wa sekta ya mifugo.
Ametoa agizo hilo leo Desemba 17, 2024 baada ya kutembelea Ranchi ya Kongwa iliyopo Wilaya ya Kongwa, jijini Dodoma huku akiahidi kurudi Januari 5, 2025 ili kuona utekelezaji wa maagizo yake.
" NARCO mnajukumu la kuzalisha mbegu bora za aina mbalimbali, Watanzania wanahitaji mifugo inayouzika kwa urahisi hapa ndani ya nchi na kimataifa tunataka kila mfugaji akiuza ng'ombe apate Sh.milioni 8 hivyo nawataka mzalishe mbegu bora kwa ajili ya wafugaji wetu," amesema Dk.Kijaji.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED