Msajili Mstaafu wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa amefariki dunia jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali za kifo chake zimetolewa leo Desemba 17, 2024 na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na kueleza kuwa wanasubiri taarifa rasmi kutoka kwa familia na wao kama ofisi ya Msajili watatoa taarifa rasmi.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu na marehemu, msiba wa Tendwa aliyehudumu katika afasi hiyo kuanzia mwaka 2001 na kuachia madaraka Agosti mwaka 2013 upo eneo la Kibamba Hospitali Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED