Dudley Mbowe kupanda kizimbani Januari

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:49 PM Dec 17 2024
Dudley Mbowe kupanda kizimbani Januari
Picha: Mtandao
Dudley Mbowe kupanda kizimbani Januari

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Kazi, Januari 6, 2025 inatarajia kuanza kusikiliza maombi ya waandishi wa habari Maregesi Paul na wenzake 9 wanaotaka Mkurugenzi wa Gazeti la Tanzania Daima, Dudley Mbowe aamuliwe kwenda gerezani kama mfungwa wa madai kwa kushindwa kulipa malimbikizo ya misharaha yao.

Mahakama hiyo mbele ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mary Mrio ilitoa uamuzi huo, leo asubuhi, Dar es Salaam, wakati shauri hilo lilipokuwa linatajwa.

Akiwakilisha wenzake Maregesi aliifahamisha Mahakama kwamba tayari hati ya wito ilishamfikia Dudley na aliahidi kufika lakini hakutokea.

Dudley alikubali kulipa fedha hizo kwa awamu tatu, Oktoba 30, Desemba 30 mwaka 2023 na awamu ya mwisho ilikuwa mwishoni mwa Februari, 2024 hakulipa na walipoingia katika makubaliano nje ya Mahakama pia kavunja makubaliano kwa kushindwa kutekeleza walichokubaliana.