Katika jitihada za kuongeza matumizi ya simu janja, Samsung Electronics East Africa imeungana na Watu Simu kuzindua kampeni inayojulikana kama ‘Samsung Kibingwa’ nchini Tanzania.
Kampeni hii itawawezesha wateja nchini kupata simu za kisasa za Samsung kutoka kwa mawakala walioidhinishwa kupitia mikopo nafuu. Wateja watahitajika kuweka amana kama itavyoelekezwa na washirika wetu Watu Simu ambapo itafuatiwa na malipo ya kila siku, wiki au mwezi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Samsung Electronics East Afrika - Tanzania, Manish Jangra amebainisha kuwa hii ni mojawapo ya jitihada ya kampuni kwa kushirikiana na wadau wake tofauti kuhakikisha kuwa Watanzania wanaweza kumiliki simu janja kwa gharama nafuu.
“Umuhimu wa matumizi ya simu unazidi kuongezeka kadri miaka inavyozidi kwenda na kuathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za kijamii na kiuchumi. Wateja wamehama kutoka kutumia simu kama kifaa cha mawasiliano mpaka kuwa nyenzo muhimu ya kiuchumi.
Kama wazalishaji wa vifaa bora vya kieletroniki kwa miaka mingi duniani tunayo fursa kubwa ya kuhakikisha watu wanapata vifaa vya kisasa na kwa gharama nafuu.
Kupitia kampeni hii, wateja wateweza kununua simu janja kwa mawakala waliodhinishwa na Samsung kupitia malipo nafuu ya mkopo ya kuanzia shilingi 1200 pekee kwa siku, wiki au mwezi kwa kipindi cha miezi 12,” alifafanua Jangra.
Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi kubwa ya Watanzania wanaotumia simu za vitochi au analogia inazidi kupungua huku wengi wakihamia kwenye matumizi ya simu janja. Takwimu zinaonyesha kuwa matumizi ya simu janja miongoni mwa Watanzania yameongezeka kutoka asilimia 15 mwezi Desemba 2021 na kufikia asilimia 32.59 mwezi Machi 2024.
Kampeni ya ‘Samsung Kibingwa’ itawanufaisha wateja nchi nzima kwa kuwatengenezea fursa ya kuwasiliana kutumia simu janja pamoja na kupata ufahamu zaidi kuhusu mkopo wa simu na namna wanavyoweza kunufaika nao.
Mawakala walioidhinishwa na Samsung pia watakuwepo katika shughuli zitakazokuwa zinaendelea mitaa ya mikoa mbalimbali kwa ajili ya mteja yeyote ambaye atataka kunufaika na aina ya mkopo mara moja.
Jangra ameongezea kuwa, “Kwa miaka mingi, Samsung imekuwa mstari wa mbele kuzalisha na kusambaza bidhaa bora za kielekitroniki nchini na ukanda wote wa Afrika ya Mashariki. Tunajivunia kuwa sehemu ya mwezeshaji wa mabadiliko inayopitia Tanzania kwa sasa ambapo wananchi wengi wanaachana na simu za analogi na kuhamia kwenye za kisasa.
Hii ni ishara nzuri kwa taifa zima kwa ujumla kuendana na kasi ya uchumi wa kidigitali duniani. Kama Samsung pamoja na kutoa teknolojia ya kisasa zaidi katika vifaa vyetu, pia tunatoa warantii ya miezi 24 na matengenezo ya kioo bure kwa mara moja chini ya mpango tunaouita ‘Samsung Care+’, hii sio tu kuonyesha imani tuliyo nayo katika ubora wa vifaa vyetu bali pia kuwaunga mkono wateja wetu kwa ujumla.”
Rumisho Shikonyi, Meneja Mkuu, Kampuni ya Watu Tanzania ameongezea kwa kusema kuwa, “Kama kampuni ya mikopo nafuu ya kifedha, tunayofuraha kuwa sehemu ya kampeni hii, ambayo itabadilisha maisha ya Watanzania kwa kiasi kikubwa. Kwetu Watu Simu, tumejizatiti katika ujumuishi wa kidijitali na kusaidia mabadiliko kutoka mitandao ya 2G/3G kwenda 4G/5G.
Simu janja sio kwamba ni vifaa tu bali ni nyenzo madhubuti zinazokuza na kuboboresha fursa za uendeshaji wa shughuli za kijamii na kiuchumi. Kupitia mikopo nafuu, tunahakikisha kila mteja anaweza kupata kifaa cha kisasa huku akiwa na uhakika wa kurejesha mkopo wake kidogo kidogo.”
Watanzania wanaweza kunufaika na kampeni hii, itakayofanyika nchi nzima, kwa kutembelea wauzaji walioidhinishwa na Samsung pamoja na maduka ya Watu Simu, mawakala, na ofisi zao ili kujipatia simu kama vile Samsung Galaxy A05, Galaxy A15, Samsung Galaxy A25 5G, Samsung Galaxy A35 5G, na Samsung Galaxy A55 5G.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED