MIAKA 48 YA CCM: Vigwaza yakemea ubaguzi,yasisitiza umoja

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 01:37 PM Feb 04 2025
Vigwaza yakemea  ubaguzi yasisitiza  umoja.
Picha: Mpigapicha Wetu
Vigwaza yakemea ubaguzi yasisitiza umoja.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Vigwaza kimeadhimisha miaka 48 ya kuzaliwa kwake, huku kikitoa wito wa kuepuka ubaguzi katika mchakato wa uchaguzi mkuu.

Mwenyekiti wa chama hicho, Athumani Kimui, ameeleza kuwa CCM haikubali kuwepo kwa ubaguzi baina ya wanachama wake, akisisitiza kwamba uchaguzi wa viongozi unapaswa kufanywa kwa kuzingatia sifa zao, badala ya kutegemea vipengele vingine vya kibaguzi.

Kimui ameongeza kuwa chama hicho, tangu kuanzishwa kwake, hakijawahi kuwa na ubaguzi, na amesisitiza kwamba jambo hili linapaswa kuendelea kulaaniwa. Amesisitiza pia umuhimu wa vikao vya chama vinavyopangwa kwenye kalenda rasmi, kwani vikao hivyo vitasaidia kuimarisha chama, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

1

Diwani wa Vigwaza, Mussa Gama, ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa kituo cha afya Vigwaza, na kueleza kuwa kabla ya kutolewa kwa fedha hizo, kata hiyo haikuwa na kituo cha afya, na wananchi walikuwa wakilazimika kusafiri hadi Mlandizi au Tumbi kupata huduma za afya. Aliongeza kwamba, kwa sasa, wanachama wa chama hicho wanashiriki kwa furaha katika harambee ya ujenzi wa ofisi ya CCM na kupanda miti kwenye kituo hicho cha afya.

Hizi ni juhudi ambazo zinaonyesha umoja na dhamira ya CCM katika kuboresha huduma za kijamii na kuhakikisha kuwa demokrasia ya chama inakuwa na misingi imara.

2