Mtinika atinga Soko la rangi tatu

By Restuta James , Nipashe
Published at 07:57 AM Jun 06 2024
Meya wa Temeke, Abdallah Mtinika, akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mbagala Rangi Tatu
Picha: Restuta James
Meya wa Temeke, Abdallah Mtinika, akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mbagala Rangi Tatu

MEYA wa Temeke, Abdallah Mtinika, ametembelea Soko la Mbagala Rangi Tatu ambako amefanya kikao kazi na kusikiliza makundi ya wafanyabiashara, mama lishe na wanamichezo.

Katika ziara hiyo Meya Mtinika ameambata na Diwani wa Charambe, Twahir Kamona.

Miongoni mwa kero zilizoibuliwa ni mama lishe kusumbuliwa pamoja na choo cha soko hilo kutotumika kwa miezi mitano zimetatuliwa na tayari choo kimeanza kutumika.

Timu ya soko hilo imemwomba Mtinika awe mlezi wao na kuomba kupatiwa jezi, ombi ambalo amelikubali na kuahidi kuwasaidia kwa hali na mali.