Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha limeidhinisha bajeti ya shilingi bilioni 39.6 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 katika kikao maalum kilichofanyika Januari 24, Mlandizi, Kibaha.
Mwenyekiti wa Halmashauri, Erasto Makala, alisema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 30 zinatarajiwa kutoka Serikali Kuu, shilingi bilioni 4.6 kutoka mapato ya ndani, na shilingi bilioni 4 kutoka kwa wafadhili.
Miradi inayotarajiwa kutekelezwa
Fedha za ndani zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:
Makala amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024, Halmashauri ilipokea shilingi bilioni 32.8, sawa na asilimia 97 ya makadirio ya mwaka ambayo yalikuwa shilingi bilioni 33.9. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya sekondari na kuanzishwa kwa ujenzi wa soko la kisasa.
Wito wa Madiwani na Mpango wa Utekelezaji
Madiwani wametoa wito kwa Halmashauri kuhakikisha barabara za mitaa zinakarabatiwa na kuongeza vyumba vya madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri, Shukuru Lusanjala, ameahidi kuwa bajeti hiyo itatekelezwa kama ilivyopangwa kwa manufaa ya wananchi. Pia alisisitiza kuwa maeneo yaliyo na changamoto za barabara mbovu, upungufu wa madawati, na vyumba vya madarasa yatazingatiwa katika utekelezaji wa bajeti hiyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED