Mnyukano CHADEMA washika kasi, Mrema acharuka

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:40 PM Jan 24 2025
MKURUGENZI wa Itikadi,Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),John Mrema.
Picha:Mtandao
MKURUGENZI wa Itikadi,Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),John Mrema.

MKURUGENZI wa Itikadi,Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),John Mrema, amesema kuwa anatishiwa kufutwa uanachama kwa maelekezo ya viongozi wake.

Kwa mujibu wa ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa X amesema: "Nimejulishwa na Mwenyekiti wa Tawi langu ameagizwa anifute uanachama kabla ya kesho ili kama nitaendelea na nia yangu ya kuzungumza na vyombo vya habari basi niwe sio mwanachama! 

Nimeshangaa sana maagizo hayo na mpango huo ambao unaratibiwa  na Viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Kata ya Segerea bwana Kitomary! 

Wanademokrasia,wameshinda Uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme! Wanataka kufukuza wengine uanachama ili wasisemwe! 

Demokrasia ni pamoja na uhuru wa Mawazo na kutoa maoni! 

Chadema,ndio Chama changu ,sijawahi kuwa mwanachama wa Chama kingine chochote! 

Nawatahadharisha acheni ujinga huo! 

Jana katika ukurasa huo,Mrema aliandika kuwa atazungunza na waandishi wa habari kwa kinywa kipana sana huku akipinga udhalilishaji unaoendelea na kwamba kuendesha chama si kuishi ughaibunu.