Maandalizi Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika yakamilika

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:37 AM Oct 07 2024
Maandalizi Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika yakamilika
Picha:Mpigapicha Wetu
Maandalizi Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika yakamilika

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio jana ameongoza kikao cha maandalizi cha Wataalam kutoka Tanzania watakaoshiriki Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika (Afrika Oil Week). Kikao kimefanyika Jijini Cape Town nchini Afrika Kusini.

Kongamano hilo litafanyika kuanzia leo tarehe 07 hadi 10, Oktoba, 2024 nchini humo.

Maudhui ya Kongamano hilo ni pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala katika Bara la Afrika.