Namungo, Tabora United, vinara kuzawadiwa penalti Ligi Kuu

By Adam Fungamwango , Nipashe
Published at 11:36 AM Oct 07 2024
Timu ya Namungo FC, na Tabora United.
Picha:Mtandao
Timu ya Namungo FC, na Tabora United.

TIMU za Namungo FC, na Tabora United, zinaongoza kwa kupewa penalti kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka sasa.

Timu hizo zimezawadiwa penalti tatu kila moja, kati ya matuta 14 ambayo yameshatolewa mpaka sasa kwenye Ligi Kuu.

Hata hivyo, pamoja na kupewa penalti hizo, Namungo imekosa mbili na kupata moja tu, huku Tabora United ikipata mbili na kukosa moja.

Kwa mujibu wa takwimu za dawati la Nipashe Digital Michezo, Namungo ilipata penalti katika mchezo wao dhidi ya Tabora United. na ukawekwa wavuni na Djuma Shaaban, aliyeiongoza timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1, lakini, Amza Mubarack alikosa tuta timu hiyo ilipochapwa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate, na Djuma alikosa katika mchezo ambao Namungo ilicheza dhidi ya Coastal Union, lakini ikashinda mabao 2-0.