Kigogo CHADEMA ashinda uchaguzi akiwa mahabusu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:21 AM Oct 07 2024
ALIYEKUWA Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob
Picha:Mtandao
ALIYEKUWA Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob

ALIYEKUWA Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob, ameshinda nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kupata kura 60, sawa na asilimia 77, akiwa mahabusu gerezani.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa Kanda ya Pwani, Kerenge Jerry alisema mshindani wake wa karibu, Gervas Lyenda alipata kura 17 sawa na asilimia 23. Wengine waliochaguliwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA (BAZECHA), James Haule, Makamu Mwenyekiti, Wilson Katunzi, huku Katibu akichaguliwa Deogratius Kajula. 

Mwekahazina ni Florence Kasilima, Mwenyekiti Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Joyce Mwabamba, Makamu Mwenyekiti, Husna Masoud, huku Katibu akichaguliwa Evangelina Marcel na Mwekahazina, Grace Mgonjo. 

Kwa upande wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA), Mwenyekiti ni Juma Juma, Katibu Lilian Byebalilo na Mwekahazina, Alex Daniel.