EU, EAC wazindua miradi mikubwa ya kukuza biashara

By Getrude Mpezya , Nipashe
Published at 01:16 PM Feb 10 2025
EU, EAC wazindua miradi mikubwa ya kukuza biashara.

Umoja wa Ulaya (EU), kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), umezindua miradi mitatu mikubwa inayolenga kuimarisha muungano wa kikanda, kukuza biashara, na kuchochea maendeleo jumuishi ya kiuchumi.

Miradi hiyo, inayofadhiliwa kwa EUR milioni 8 kutoka EU, inalenga kuondoa vikwazo vya biashara, kuimarisha utekelezaji wa sheria za ushindani, na kuongeza uwezo wa taasisi za EAC. Aidha, miradi hiyo inatoa msukumo maalum kwa uwezeshaji wa wanawake na vijana ili kuwajengea nafasi bora za kiuchumi.

Mkuu wa Ushirikiano katika Ofisi ya EU kwa Tanzania na EAC, Marc Stalmans, amesema kuwa miradi hiyo ni sehemu ya mkakati wa EU wa kusaidia muungano wa kikanda kupitia Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) na Mpango wa Team Europe. Lengo kuu ni kujenga uchumi thabiti na jumuishi zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.