Bolt yazindua huduma Kilimanjaro, kuimarisha usafiri kwa wakazi,watalii

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:35 PM Jan 24 2025
Bolt yazindua huduma Kilimanjaro, kuimarisha usafiri kwa wakazi,watalii.
Picha: Mtandao
Bolt yazindua huduma Kilimanjaro, kuimarisha usafiri kwa wakazi,watalii.

Bolt, jukwaa la usafiri linaloongoza barani Afrika na Ulaya, sasa limezindua rasmi huduma zake mjini Moshi kama sehemu ya mpango wake wa kupanua shughuli zake kote Tanzania.

Hatua hiyo inaonyesha dhamira ya Bolt ya kutoa huduma za usafiri salama, nafuu, na za kuaminika kwa jamii, pamoja na kuboresha upatikanaji wa suluhisho muhimu za usafiri.

Mkoa wa Kilimanjaro, makazi ya kilele kirefu zaidi barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, na kitovu chenye shughuli nyingi kwa wakazi wa ndani na watalii wa kimataifa, sasa wanufaika na aina rahisi ya usafiri la Bolt. Uzinduzi huo unaendana na mahitaji yanayoongezeka jijini Moshi kwa suluhisho za kisasa na za aina mbalimbali za usafiri zinazokidhi ongezeko la idadi ya watu na ukuaji wa sekta ya utalii.

Kufika kwa Bolt mjini Moshi kunaleta manufaa kadhaa kwa jamii, ikiwa ni pamoja na: Mamia ya nafasi za ajira kwa madereva wa ndani, utunzaji wa mazingira kwa kuongezeka kwa matumizi ya pikipiki za umeme, kama ilivyoanza kwa mafanikio jijini Arusha, na usafiri wa uhakika unaohamasisha harakati zaidi kwa wapenzi wa safari na matukio.

Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania, alisema kuwa jukwaa hili la usafiri lina mpango wa kupanua huduma zake katika maeneo mengine ambako utalii ni sekta kuu, huku madereva wa ndani na biashara zikinufaika kutokana na ongezeko la huduma za usafiri.

1

  “Kwa kawaida, watalii wanathamini sana usalama na nauli wanapotafuta usafiri wa ndani. Wanapendelea kutumia fedha zao kwenye burudani na mambo yakitamaduni badala ya kutumia muda mwingi kutafuta usafiri au kubaki hotelini muda mwingi kuepuka changamoto za usafiri,” alisema Kanyankole.

Kupitia upanuzi wake, Bolt inaendelea kuunga mkono juhudi kubwa za serikali katika sekta ya usafiri zinazolenga kuchochea uchumi. Mwaka 2024, Bolt ilizindua huduma zake Morogoro kufuatia uzinduzi wa reli ya kisasa ya SGR, hatua inayodhihirisha kujikita kwake katika malengo ya maendeleo ya miundombinu ya Tanzania.

Kwa kupanua huduma zake katika maeneo yanayostawi kitalii, Bolt inaendelea kuiwezesha jamii na kuchangia katika mazingira ya kiuchumi yenye mabadiliko makubwa nchini Tanzania.