Benki ya Akiba imesema itaendelea kuunga mkono serikali kwa kutoa elimu ya fedha huku ikiboresha huduma zake nchi nzima ili kusaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuchochea kukua kwa uchumi wa Taifa.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Silvest Arumasi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya elimu ya fedha yaliyojumuisha viongozi wa benki hiyo ,watumishi kutoka Wizara , taasisi na ofisi mbalimbali za serikali lengo likiwa ni kubadilishana ujuzi na kujenga mahusiano mazuri huku wakifahamiana na kuweka mikakati ya pamoja namna ya kuwahudumia watumishi wa Umma kwa weledi zaidi na kujibu maswali na kujibu maswali huku wakitatua kero zinazojitokeza kiutendaji.
"Tunaahidi kuwa benki itaendelea kuunga mkono serikali kwa kuwasadia wananchi kuwapatia mikopo nafuuu ili kuinua mitaji yao pia kupanua wigo wa huduma nchi nzima ili kufikia azma ya kutoa mchango mkubwa wa kuwepo kwa huduma shirikishi za kifedha yaani financial inclusion" alisema
Naye Upendo Makula, Meneja wa Tawi la ACB - Dodoma aliwashukuru washiriki wote kwa kuitikia mwito kwa ujumla wao.
Aidha washiriki wote waliishukuru benki hiyo kwa mada nzuri za semina hiyo na wameahidi kutumia elimu hiyo kama chachu katika utendaji wao wa kila siku kwani wamejengewa msingi imara wa uelewa wa maswala ya fedha
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED