WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe, amezindua kiwanda cha kubangua korosho Newala mkoani Mtwara.
Kwa mujibu wa Bashe, kiwanda hicho kimegharimu Sh.bilioni 3.4.Chama Kikuu cha Ushirikia cha TANECU kimeanza safari ya kuwa na ushirikia imara kwa kujenga kiwanda hicho.
Bashe ambaye yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi, amekipongeza chama cha TANECU kwa kuwa mfano mzuri wa kuonesha ushirika unaozidi kuwa imara kwa kuhakikisha uwekezaji huo wa kiwanda ni wa wakulima wenyewe.
Pia, ameelekeza kijengwe kiwanda kingine kama hicho Tandahimba na kiwe tayari msimu ujao.
Kiwanda hicho cha kubangua korosho kilichozinduliwa, kina uwezo wa kubangua tani 3,500 kwa mwaka na kwamba mkakati ni kuwa na viwanda 20 vya Kubangua Korosho chini ya TANECU katika Mkoa wa Mtwara ambapo 10 vitajengwa Newala na 10 vingine vitajengwa Tandahimba.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED