Mwenyekiti wa Simba Mkoa wa Mwanza, Is-haka Mukadam ‘Ashraf’, amefariki usiku wa kuamkia leo jijini humo, imeelezwa.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Simba imesema Ashraf, amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Klabu hiyo inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wa mpira wa miguu kwa kumpoteza mpendwa wao.
Ashraf alikuwa ni nguzo muhimu kwa Simba na alikuwa akisimamia maandalizi yote muhimu pale timu hiyo inapokwenda katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Habari zaidi zitakujia kadri tunavyoendelea kuzipokea na soma gazeti Nipashe
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED