UMEWAHI kujiuliza kuhusu muda unaotumia ukiwa faragha chooni? Huu ndio ukweli. Kwa walio wengi tabia ya kukaa muda mrefu chooni, wengine wakiwa hata na simu zao ni jambo la kawaida. Wapo wanaosoma habari tofauti kupitia simu.
Wataalamu wanatahadharisha kwamba kukaa kwa muda mrefu chooni, kunaweza kunaathiri afya yako.
Hasa hatari ya kuongezeka kwa ugonjwa wa bawasiri (hemoroidi) na misuli kuwa dhaifu ya maeneo ya chini ya tumbo.
Daktari wa binadamu, Lai Xue, mtaalamu wa upasuaji wa utumbo kutoka Chuo Kikuu cha Texas Southwestern Medical Center kilichopo Dallas, Marekani.
Bwasiri ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika njia ya haja kubwa ambayo husaidia kudhibiti kinyesi.
"Unapowasiliana na wagonjwa wangu, malalamiko ni moja ya maeneo ambayo tunapaswa kujikita nayo ni namna wanavyotumia muda mwingi chooni," anasema Xue.
Watu wanapaswa kutumia wastani wa dakika tano hadi 10 chooni, kulingana na Dk. Farah Monzur, Profesa msaidizi wa tiba na mkurugenzi wa Kituo cha Magonjwa ya Matumbo ya Stony Brook Medicine kilichopo Long Island, New York.
Kwa nini ni tatizo kama unakaa kwa muda mrefu? Kwanza, hapa kuna somo fupi la fizikia. Nguvu ya mvuto (gravity) inatufanya tuwe ardhini, lakini nguvu hiyo hiyo inailazimisha mwili kufanya kazi zaidi, ili kurudisha damu juu kwenda kwa moyo, alisema Xue.
“Kiti cha choo kilicho wazi, chenye umbo la mviringo, , kingewekwa sehemu chini ungekuwa umekaa kwenye kochi. Hivyo mvuto ukivuta nusu ya chini ya mwili chini katika sinki la choo, shinikizo linaloongezeka linaathiri mzunguko wa damu.
"Inakuwa kama valvu moja ya kuelekea upande mmoja ambapo damu inaingia, lakini damu haiwezi kutoka tena," anasema Xue.
“Hii husababisha mishipa ya damu inayozunguka sehemu ya haja kubwa na sehemu ya chini ya haja kubwa kuvimba na kujaa damu na kuongeza hatari ya kuugua hemoroidi.
Mara nyingine rangi fulani za haja kubwa zinaweza kuwa alama za hatari, kulingana na wataalamu
USIJILAZIMISHE
Kulazimisha kujisaidia pia kunaweza kuongeza shinikizo linaloleta bawasiri. Watu wanaopitia kwenye simu zao wakiwa chooni, mara nyingi hupoteza muda, wakiwa wamekaa na kulazimisha misuli yao kutoa kinyesi,” anasema Monzur.
“Madaktari wako wanaweza kusema, leo hii, tunaona ongezeko la watu wanaokaa muda mrefu chooni na hii ni hatari sana kwa viungo vya anorektali na sakafu ya pelvis," anaongeza Xue.
“Fanya kukaa kwenye kiti cha choo kuwa jambo lisilo la kuvutia, ili kuepuka kutumia muda mwingi kwenye kiti cha choo,” Dk. Lance Uradomo, mtaalamu wa magonjwa ya utumbo kutoka City of Hope Orange County huko Irvine, California.
Dk. Xue pia alipendekeza unywaji maji mengi na kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile shayiri na maharage, ili kusaidia kutoa kinyesi kawaida na kuepuka kulazimisha.
Chama cha Kitaifa cha Tiba Marekani, kinapendekeza lita 2.7 hadi 3.7 za maji kila siku.
Idara ya Kilimo ya Marekani, inapendekeza gramu 14 za nyuzinyuzi kwa kila kalori 1,000 za chakula.
Xue anasema kwamba nyuzinyuzi na maji hufanya kinyesi kuwa laini na hivyo kutoka kwa urahisi.
Shirika la Saratani la Marekani, liliripoti hivi karibuni ongezeko la viwango vya saratani ya utumbo miongoni mwa watu walio na umri wa chini ya miaka 55 tangu katikati ya miaka ya 1990 na asasi isiyo ya kiserikali ilikadiria kuwa kutakuwa na visa vipya 106,590 vya saratani ya utumbo na visa vipya 46,220 na haja kubwa mwaka huu.
CNN
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED