HIVI karibuni umaarufu wa ufahamu kuhusu kizazi kilichopo na vilivyopita, umeshika kasi hasa mitandaoni.
Kila kizazi huwa na jina lake. Hivi ndio vizazi vyenyewe kwa mujibu wa wanasayansi duniani.
Cha kwanza ni; Baby Boomers ni watu waliozaliwa kati ya 1946 na 1964.
Cha pili ni; Generation X, au Gen X, ni kundi la watu waliozaliwa kati ya katikati ya miaka ya 1960 na mwishoni mwa miaka ya 1970.Cha tatu ni; Millennials ni kizazi cha watu waliozaliwa kati ya mwanzoni mwa miaka ya 1980 na katikati ya miaka ya 1990.Cha nne ni; Generation Z (Gen Z) ni kizazi cha watu waliozaliwa kati ya mwishoni mwa miaka ya 1990 na mapema 2010.Cha tano ni; Generation Alpha, ni kundi la waliozaliwa kati ya mwaka 2010 na 2024. Sasa kuna kizazi kipya, baada ya kuingia mwaka 2025. Hiki ni cha sita; Gen Beta, ni kizazi cha watu waliozaliwa kati ya 2025 na 2039. Upo kundi gani? Chanzo: CBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED