WATU wote wanaomiliki pasipoti kutoka barani Afrika, sasa wanaweza kuzuru Ghana bila kuhitaji Visa.
Rais anayemaliza muda wake, Nana Akufo-Addo, amesema.
Alitangaza mpango huo mwezi uliopita, lakini katika hotuba yake ya mwisho ya hali ya taifa siku ya mwishoni mwa wiki, alisema kuwa sera hiyo ilianza kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka.
Usafiri bila Visa ndani ya bara hilo, kwa muda mrefu umekuwa ni hamu kwa wale wanaokuza maadili ya Uafrika na inaonekana kuwa muhimu kwa ushirikiano wa kiuchumi.
Ghana, sasa ni nchi ya tano barani Afrika kutoa ulazima wa kuwa na Visa, kwa wasafiri kutoka bara zima.
Nchi nyingine ni Rwanda, Ushelisheli, Gambia na Benin.
"Ninajivunia kuidhinisha safari bila Visa kwenda Ghana kwa wamiliki wote wa pasipoti wa Kiafrika, kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu," Akufo-Addo aliwaambia wabunge katika hotuba yake ya mwisho bungeni kabla ya kujiuzulu wiki ijayo, baada ya miaka minane mamlakani.
Kwa mujibu wa Akufo-Addo hayo yote ni mambo muhimu katika utekelezaji wa Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika, ambayo inatazamia kuwa na Afrika iliyounganishwa ifikapo 2063.
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED