NAOMI Osaka (27), amejiondoa katika fainali ya Auckland Classic, akiwa na maumivu ya tumbo. Hilo ni pigo kwa staa huyuo wa Kijapani, ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuanza kwa Australian Open.
Akiwa anacheza fainali yake ya kwanza ya WTA, baada ya miaka mitatu, dhidi ya Clara Tauson kutoka Denmark, bingwa wa Grand Slam mara nne alimuomba daktari, baada ya kushinda seti ya kwanza 6-4 na aliondoka uwanjani muda mfupi, hii leo.
Osaka kujitoa ghafla kutoka kwenye huku akijiandaa na Australian Open, lilikuwa pigo kwa wengi, kwani alicheza bila matatizo yoyote kwenye seti ya kwanza ya dakika 35, akionesha makali yake kwa kupiga michomo mikali na kumvunja mpinzani wake kwenye mchezo ya tatu na tano.
Wakati wa kubadilishana, Osaka, alisimama na kufanya mazoezi kadhaa ya kunyoosha mwili akiwa kwenye mapumziko ya matibabu.
Baada ya kushauriana na mtaalamu wa tiba, alimshika mkono Tauson, ambaye alishinda taji lake la tatu la kazi na la kwanza tangu mwaka 2021.
Osaka hakufichua kile kilichosababisha kujitoa kwake katika mahojiano mafupi aliyofanya pembeni ya uwanja.
ALJAZEERA
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED