Waziri wa Fedha Zanzibar, Juma Maliki Akili amesema mpango wa serikali hiyo ni kukopa na kulipa madeni kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini na sio kusubiri fedha za misaada mabao wakati mwingine huchelewa.
Waziri huyo aliyasema hayo juzi alipokuwa kiongea na waandishi wa habari na kusisitiza wanaokwenda mahali huko kwaajili ya uwekeaji katika viwanda na sekta ya utalii kukiwa na huduma za kibenki zitasaiida juhudi za Zanzibar kupatia huduma nafuu zitakazo fanikisha kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
“Tunakuza uchumi kupitia shughuli za uwekezaji ujenzi na za kifedha, shughuli hizi zimechachua sana uchumi wa wananchi na kusaidia kuondoa tatizo la ajira pamoja na kwamba bado lipo kwa kiasi.
Nitoe wito kupitia tawi jipya la benki ya KCB tuzingatie sana kutengeneza pia ajira kwa vijana wenye taaluma na wanakosa nafasi hizo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Balozi Peter Kallaghe, alisema hatua ya kuweka tawi hilo inahakisi dhamira ya kukuza uchumi jumuishi, kuharakisha mageuzi ya sekta ya fedha, kuendeleza uchumi wa buluu, kuiwezesha sekta binafsi na kutumia teknolojia kama kichocheo cha maendeleo ya kifedha na jamii.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED