Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka msisitizo wa kuimarisha umoja, mshikamano na upendo kama msingi wa kulinda amani na kuharakisha maendeleo ya taifa, huku kikiahidi kuendelea kuwa karibu na wananchi na kusikiliza changamoto zao.
Wito huo umetolewa na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi, anapoanza ziara yake ya siku tatu mkoani Tabora.
Akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo jipya la CCM lililogharimu zaidi ya Sh. milioni 100, ameeleza kuwa uhai na uimara wa chama hicho unaonekana wazi kwa vitendo.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kuilinda amani ya nchi, akisisitiza kuwa amani ndiyo nguzo ya maendeleo anaeleza kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani na ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha utulivu unaendelea kudumu bila kuyumbishwa na watu wachache wenye nia ovu.
Ziara hiyo pia itahusisha ukaguzi wa miradi ya maendeleo, mikutano ya hadhara pamoja na kukutana na mabalozi wa chama katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mawasiliano kati ya chama na wananchi.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED