Samia: W’biashara waliokuwapo kabla soko kuungua wawe kipaumbele

By Pilly Kigome , Nipashe Jumapili
Published at 03:48 PM Feb 08 2026
Baadhi ya wananchi kwenye uzinduzi huo
Picha: Mpigapicha Wetu
Baadhi ya wananchi kwenye uzinduzi huo

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema wafanyabiashara ambao kabla soko halijaungua Julai 10, 2021 ndio wapewe kipaumbele, kwa kupatiwa nafasi sokoni.

Amesema kunatakiwa usawa na kuleta uwiano kupata nafasi za kufanyia biashara na kuwataka waache makundi kwakuwa soko hilo ni la watu watanzania wote si la mtu binafsi.

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa soko jipya la Kariakoo leo, Februari 8, 2026 jijini Dar es Salaam.

Pia Rais Samia Suluhu Hassan, amewaonya viongozi wenye nia ya kuhodhi maeneo ya soko jipya Kariakoo, akidai mbinu hiyo hulenga kupangisha watu wao.

“Halafu ninyi ndio mnakuja kupangisha watu!’

Akitoa maelekezo hayo Rais Samia amesema kuwa anataka kuona wafanyabiashara waliokuwa wanafanya biashara awali katika soko kabla halijaungua Julai 10, 2021 wapewe kipaumbele kupatiwa nafasi sokoni hapo.

"Nisingependa kuona viongozi mnahodhi maeneo haya halafu ninyi ndio mnakuja kupangisha watu na kuweka watu wenu na kuwaonea ambao walikuwa wanafanya biashara awali, tuweke watu kwa usawa maana hiki sio mali yenu ni maki ya wananchi" amesisitiza Rais Samia.

Pia Rais Samia amelitaka Shirika la Masoko Kariakoo kuweka mifumo ya kisasa ya ulipaji kodi, mapato na matumizi iwe ya uwazi ili kuepusha ubadhirifu kutoka sokoni hapo.

Amesema mifumo hiyo italeta tija kwakuwa hakutakuwa na malalamiko ya tozo na ada kwa wafanyabiashara kukandamizwa kwa ulipaji kodi na hakutakuwa na mabavu ya kugombana na wafanyabiashara kuhusu ulipaji kodi.

"Kaeni kwa pamoja wafanyabiashara na viongozi mkubaliane kila upande kusiwe nanupande ambao utamuumiza mwenzie kodi zisiwe juu sana na zisiwe chini sana" ameagiza