Samia aagiza ulinzi miundombinu Kariakoo aonya upendeleo

By Christina Mwakangale , Nipashe Jumapili
Published at 02:55 PM Feb 08 2026
Rais Samia Suluhu Hassan, akizindua soko hilo
Picha: Mtandao
Rais Samia Suluhu Hassan, akizindua soko hilo

Rais Samia Suluhu Hassan, amezindua Soko la Kariakoo, huku akisisitiza upangishaji wa maeneo ya kufanyia biasha usiwe wa upenmdeleo.

Amesema asingependa kusikia wafannyabiashra waliopangishwa eneo hilo, kwa ajili ya biashara, kupangishwa kutokana na upendeleo kutoka kwa viongozi.

“Shirika la Masoko Kariakoo lifanye kazi yake ipasavyo. Naagiza TRA kuhakikisha utozaji kodi ni wa uhalali, pia mifumo ya ukusanyaji mapato iunganishwe na mfumo wa kidijitali wa serikali.”

Kadhalika Rais Samia, amesisitiza utunzaji wa miundombinu ya soko hilo, kwa kuwa fedha zilizotumika kwenye ujenzi ni za watanzania.

Soko hilo linahudumia nchi mbalimbali hasa majirani, ni kama vile Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Rwamba na Burundi.

Takribani watu 200,000 wanahudumiwa kila siku huku wafanyabiashara 1,520 wamethibitishwa kufanya kazi kwenye jengo hilo jipya. Jengo hilo lina gorofa sita na miundombinu ya kisasa.